Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiangalia kilula cha maji cha mradi wa Liula,
Wilaya ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoa maagizo kwa watendaji mara baada ya
kukagua Tenki la maji la mradi wa Parangu katika Wilaya ya Songea
Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso akitoka kukagua chanzo cha maji cha Masimeli,
kinachotumika kuzalisha maji kwa ajili ya mradi wa Lipaya katika Wilaya
ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye tenki la mradi wa Matimila, Wilaya
ya Songea Vijijini, mkoani Ruvuma.
……………………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Jumaa Aweso amesema kuwa anakerwa na wakandarasi wasio na
uwezo, ambao wamekuwa wakitekeleza miradi bila kuzingatia mikataba, ama
kutoikamilisha kwa wakati au kutekeleza chini ya kiwango kwa kukosa
thamani halisi ya fedha iliyotumika.
Aweso alisema hayo wakati
akikagua utekelezaji wa miradi ya maji katika Wilaya ya Songea Vijjini,
katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma na kusikitishwa na mwenendo wa
utekelezaji usioridhisha wa baadhi ya miradi.
Naibu Waziri alisema kuwa ipo
haja ya kufutiwa usajili na kutokupewa kazi yoyote nchini wakandarasi
wote wababaishaji, baada ya kutoridhishwa tendaji wao katika baadhi ya
miradi wilayani humo.
‘‘Hatutawavumilia wakandarasi
wasio na uwezo ambao wanatuangusha, tutawafuatilia na ikiwezekana
wafutiwe usajili kabisa nchini ili wasiendelee kufanya kazi mahali
popote nchini, tubaki na wakandarasi wenye uwezo’’, alisema Aweso.
Akiwa mkoani Ruvuma, Aweso
ametembelea miradi mbalimbali ya maji inayotekelezwa katika wilaya za
Tunduru, Namtumbo, Songea Mjini, Songea Vijijini na Madaba lengo likiwa
ni kuweka msukumo katika utekelezaji wa miradi kwa nia ya kuhakikisha
inakamilika kwa wakati na wananchi wa mkoa huo wanapata huduma ya maji
ya uhakika
EmoticonEmoticon