Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati
akikagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya
Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma,
Wengine Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Pololet Kamando Mgema
(Kushoto) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Katikati) na Meneja NFRA Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya, Jana Novemba 2, 2017. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na kina mama
waliojipatia kibara kwenye ujenzi wa Kituo cha mafunzo ya kilimo OTC
Lilambo kitakachojihusisha na uchakataji wa mahindi kilichopo Mtaa wa
Namanditi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea wakati wa ziara ya kikazi
ya siku moja Mkoani Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Wa tatu Kushoto)
akitembelea na kukagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula
Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma, Wengine
Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe (Kushoto) Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Wa (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Wa Pili kulia) na Meneja NFRA Kanda ya Songea, Jana Novemba 2, 2017.
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alipotembelea Kijiini Likuyu Fusi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya Songea Mjane Bi Ester Gama ambaye ni mke wa Marehemu Leonidas Gama akimvisha kitenge ikiwa ni ishara ya upendo na faraja. Gama alifariki Dunia Novemba 23, 2017 katika Hospitali ya Mtakifu Joseph ya Peramiho.
Jana Novemba 2, 2017.
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua mahindi ili
kubaini alipotembelea Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula
Kanda ya Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa
Ruvuma, Jana Novemba 2, 2017.
Naibu
Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisisitiza jambo wakati
akikagua Maghala ya Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula Kanda ya
Songea (NFRA) wakati wa ziara ya kikazi Wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma,
Jana Novemba 2, 2017.
Na Mathias Canal, Ruvuma
Uongozi
Wa Mkoa Wa Ruvuma leo Disemba 1, 2017 umeelekezwa kuwahamasisha
wakulima kujiunga na vyama vya msingi vya ushirika kwani kupitia vikundi
ndio njia muhimu na mkombozi kwa manufaa ya mkulima mmoja mmoja na
Taifa kwa ujumla.
Amebainisha
hayo Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa wakati
akizungumza na baadhi ya wakulima sambamba na viongozi Wa wakulima
katika Mkutano Wa hadhara ulifanyika katika eneo la Ofisi za Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula Kanda ya Songea.
Pamoja
na kuwasisitiza wakulima hao kujiunga katika vikundi vya vyama vya
msingi vya ushirika, Mhe Naibu Waziri ameelekeza uongozi Wa Mkoa Wa
Ruvuma kutilia msisitizo umuhimu Wa Vyama hivyo kwani ni maelekezo ya
ilani ya Ushindi ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha miaka mitano
2015-2020 inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ikiongozwa na Mhe
Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema
kuwa vikundi hivyo vikianzishwa na kuwa na Uongozi vitarahisisha kuuza
mazao mazuri kwani kutakuwa na nguvu ya pamoja inayowakutanisha kwa
kuongozwa na sheria na taratibu walizojiwekea kama kikundi pasina kuwa
kinyume na taratibu za serikali.
"Upo
umuhimu mkubwa Wa kujiunga na AMCOS kwani ni jambo lisilokuwa la hiari
ambapo itarahisisha kupata mikopo huku kwa serikali ikiwa ni njia rahisi
kuwahudumia, Aidha Elimu inapaswa kutolewa juu ya umuhimu Wa Vyama vya
msingi vya ushirika" Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Aliongeza
kuwa Mamlaka ya Taifa ya Hifadhi ya Chakula nchini inapaswa pia kutoa
Elimu kwa umma juu ya majukumu yake kwamba ni kununua mahindi na
kuyahifadhi ili kuwa na akiba pindi panapotokea Ukame serikali iweze
kuwahudumia.
Awali
Naibu Waziri Wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alitembekea na kukagua Ghala
La kuhifadhi mahindi Kanda ya Songea ambapo ameshuhudia akiba ya kutosha
ya mahindi ambapo mpaka kufikia Leo Disemba 2, 2017 Kanda ya Songea ina
mahindi yanayofikia Tani 21,892.924 huku kati yake Tani 10,335.395 ni
ununuzi Wa msimu Wa mwaka 2016/2017 na Tani 11,557.529 ni ununuzi Wa
mwaka huu 2017/2018.
Aidha,
Mhe Mwanjelwa amezuru Kijiini Likuyu Fusi, Kata ya Lilambo, Wilaya ya
Songea na kutoa pole kwa Ndugu na Jamaa akiwemo Bi Ester Gama ambaye ni
mke Wa aliyekuwa Mbunge na Diwani wa Songea Mjini Mkoani Ruvuma,
Marehemu Leonidas Gama aliyefariki Dunia Novemba 23, 2017 Majira ya saa
4:25 Usiku katika Hospitali ya Mtakifu Joseph ya Peramiho iliyopo Songea
baada ya kukimbizwa huko kwa matibabu baada ya kuugua ghafla.
EmoticonEmoticon