Meneja mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mapema leo kuhusu ofa mpya ya 'Simu Janja kwa Mpango' kutoka Tigo katika msimu huu wa sikukuku. Wateja wa Tigo wana fursa ya kupata simu za smartphone bure kwa njia rahisi kupitia menu mpya ya *147*00# kwa kununua bando au kwa kulipia kidogo kidogo.Kulia ni Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh. |
Pata Simu za Smartphone BURE kutoka Tigo katika msimu
huu wa sikukuuu!
Dar es Salaam, Novemba 28, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo
Tanzania, leo imetangaza dili za kipekee zinazohusu simu za Smartphone ambazo
zitahakikisha kila mtu anakuwa sehemu ya maisha ya kidigitali katika msimu huu
wa Krismasi na mwaka mpya.
Akitangaza ofa hizo za msimu wa sikukuu Dar es Salaam
leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa Tigo, David Umoh alisema dili hizo kemkem
zinapatikana kwa kupiga namba ya menu mpya *147*00# na kubonyeza kitufe cha ‘Duka la Simu’ ili
kuchagua simu unayoipenda, na kisha kutembelea Duka lolote la Tigo nchi nzima
ili kuchukua simu uliyoichagua.
‘Katika
ofa ya kwanza, wateja wa Tigo wanaweza kupata simu ya Smartphone BURE kirahisi
kwa kununua bando kuanzia TZS 25 000
ambayo - pamoja na Smartphone ya bure – inawapa 1GB data, SMS 50 na dakika 50 za
kupiga Tigo – Tigo,’ alisema.
Katika
dili ya pili, wateja wa Tigo pia wanaweza kupata Smartphone kwa kuchagua mpango
wa kulipia kwa miezi sita. Ofa hii inawahusu wateja wa sasa wa Tigo ambao
wanakidhi vigezo vilivyowekwa.
Katika
msimu huu wa sikukuu, Tigo pia inatoa ofa ya ‘Lipia sasa, Chukua Baadaye’
ambapo wateja wanaruhusiwa kuchagua simu yoyote ile wanayoipenda na kisha
kufanya malipo ya awamu kila mwezi, ambapo wataruhusiwa kuchukua simu
waliyoichagua baada ya kumaliza mpango wa malipo ya kila mwezi.
‘Kupitia ofa hizi kabambe, Tigo inaendelea kushika
hatamu za ubunifu unaoendana na mahitaji ya wateja kwa kuwezesha kila mtu
kumiliki mojawapo ya hizi simu bomba za Smartphone, ambazo zimeunganisha na
mitandao ya jamii. Hii ndio njia yetu ya kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa
sehemu ya maisha na mabadiliko ya kidigitali yanayoongozwa na Tigo,’ David alisema.
‘Tunawakaribisha wateja wetu wachangamkie ofa hizi za
kipekee katika msimu huu wa sikukuu kwa kujigiftisha au kuwagiftisha ndugu,
jamaa na marafiki kwa simu hizi bora za smartphone. Simu zote zinakuja na
mpango rahisi wa malipo, bando murwa na ofa za kipekee ambazo zitahakikisha
kila mtu ataweza kufurahia na kutunza kumbukumbu za shamrashamra za sikukuu
katika simu yake mpya ya smartphone kutoka Tigo.’
EmoticonEmoticon