Meza
Kuu wakiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) (wa pili kushoto) wakiimba Wimbo wa Taifa wakati wa Mahafali
ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM, yaliyofanyika katika ukumbi
wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam ambapo wanafunzi 2692
wamehitimu kozi mbalimbali katika Nyanja za Fedha, Uhasibu, Bima, TEHAMA
na Hifadhi ya Jamii. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho
Prof. Lettice Rutashobya na wa Pili kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Prof.
Tadeo Satta.
Mkuu
wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Prof. Tadeo Satta, akihutubia wakati
wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM, yaliyofanyika
katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam, ambapo wanafunzi
2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha, uhasibu, bima,
TEHAMA na hifadhi ya jamii.
Mwenyekii
wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Prof. Lettice Rutashobya,
akihutubia wakati wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM
yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam,
ambapo wanafunzi 2692 wamehitimu kozi mbalimbali katika nyanja za fedha,
uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
Baadhi
ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM,
yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam,
wakifuatilia kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa
mahafali hayo ambayo Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango,
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb).
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha- IFM
yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jijini Dar es Salaam,
Dkt. Philip Isdor Mpango Mb), akihutubia Jumuiya ya wanachuo hicho
ambapo aliwatunuku vyeti wanafunzi 2692 waliohitimu kozi mbalimbali
katika nyanja za fedha, uhasibu, bima, TEHAMA na hifadhi ya jamii.
Wanafunzi
wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, waliofanya vizuri zaidi katika
masomo yao wakipokea zawadi ya hundi kifani yenye thamani ya shilingi
1,200,000 ambayo ni sehemu ya zawadi lukuki walizopewa wakati wa
Mahafali ya 43 ya Chuo hicho, yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond
Jubilee, Jijini Dar es Salaam.
Mhitimu
Bi. Elizabeth Mnzava akipokea zawadi ya cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi
katika Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb) baada ya kufanya vizuri katika masomo yake.
Sehemu
ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM,
wakinyanyua juu kofia zao kwa furaha kuashiria kumaliza sehemu ya safari
yao ya kimasomo, baada ya kutunukiwa vyeti na shahada nyingine
mbalimbali, katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa wahitimu ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja akionesha
furaha isiyo kifani baada ya kutunukiwa Shahada yake baada ya kuhitimu
masomo katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM, Jijini Dar es Salaam,
ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (Mb).
Sehemu
ya wahitimu wa Mahafali ya 43 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha-IFM,
wakinyanyua kofia zao juu kwa furaha baada ya kutunukiwa shahada zao
wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee
Jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amewaonya wahitimu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha IFM kuacha tamaa ya kutaka kupata mali za haraka
haraka na kutojihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi wawapo kazini
ili waweze kuisadia nchi kufikia maendeleo ya haraka.
Dokta
Mpango aliyasema hayo wakati akiwatunuku vyeti vya kozi mbalimbali
wahitimu 2692 wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, wakati wa mahafali ya
43 ya Chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa moja ya changamoto zinazoikabili jamii hivi sasa ni mmomonyoko wa
maadili katika utumishi wa Umma hali iliyosababishwa na suala la rushwa
na ufisadi kuota mizizi na kuwa tatizo kubwa katika jamii.
“Katika
miaka ya karibuni kumekuwa na matatizo mengi ya matumizi mabaya ya
fedha za umma ikiwemo watumishi hewa, wanafunzi hewa na pembejeo hewa,
nawataka wahitimu mkafanyekazi zenu kwa kuzingatia maadili na kuepuka
tabia ya kutaka utajiri wa harakaharaka” Alisisitiza Dkt. Mpango.
Dkt.
Mpango alitumia fursa hiyo pia kuelezea mafanikio makubwa yaliofikiwa
nchini katika sekta ya fedha katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini
kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma, mikopo ya mitaji ya kuwekeza
katika Sekta mbalimbali na kuhakikisha kuwa sekta hiyo inabaki imara.
Alisema
kuwa kutokana na hatua hizo, idadi ya taasisi za fedha imeongezeka
kutoka 31 zilizokuwepo mwaka 1999 hadi kufikia 67 Novemba mwaka 2017
huku taasisi hizo zikiwafikia watu wengi zaidi hadi pembezoni mwa miji
hata vijijini.
“Sekta
ya Bima nayo imepiga hatua ambapo kampuni zilizosajiliwa zimefika 31,
wakala wa bima 124 kutoka wakala 1 iliyokuwepo miaka ya 70 huku ukwasi
katika kampuni hizo ukiongezeka kutoka asilimia 47.1 mwezo Juni 2016
hadi kufikia asilimia 49.8 mwezi Juni, 2017.
Alisema
kuwa licha ya mafanikio hayo, taasisi za fedha zimekuwa zikiathiriwa na
uwepo wa mikopo chechefu iliyoongezeka hadi kufikia asilimia 10.74
mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 9.07 mwaka 2016 na kutoa wito kwa
wahitimu hao kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto kama hizo na
kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kwa kuzingatia mahitaji ya Taifa ili
kuondokana na umasikini.
Aidha,
Dokta Mpango alisema kuwa Serikali itaendelea kugharamia mikopo ya
wanafunzi wa elimu ya juu wenye uhitaji ambapo katika Bajeti ya Mwaka
huu, imepanga kutumia zaidi ya shilingi bilioni 427.54 kwa kazi hiyo kwa
kuwalipia ada na gharama nyingine za masomo wanafunzi 122,623.
Mwenyekiti
wa Baraza la Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM Prof. Lettice Rutashobya
ameiomba Serikali kukisaidia Chuo hicho kwa kukipatia fedha ili kiweze
kujiimarisha na kuendelea kutoa taaluma bora ya masuala ya fedha,
uhasibu, bima, TEHAMA na Hifadhi ya jamii huku Mkuu wa Chuo hicho Prof.
Tadeo Satta akisema kuwa chuo hicho kimejipanga kujenga kampasi mkoani
Pwani na mkoani Dodoma ikiwa ni mikakati ya kuongeza uwezo wa kudahili
wanafunzi wengi zaidi.
Aidha
viongozi hao wa Chuo cha IFM waliiomba Serikali kutenga shilingi bilioni
2 kila mwaka katika Bajeti ya Serikali ili waweze kuzitumia kujenga
kampasi hizo mbili, moja katika eneo la Msata mkoani Pwani na nyingine
inayotarajiwa kujengwa mkoani Dodoma.
“Katika
hatua za awali wakati tunataka kutumia eneo la ekari 50 tulilolipata
mkoani Dodoma, Chuo kimepanga kuanza kutoa mafunzo ya shahada ya uzamili
katika fani ya fedha na uwekezaji kwa kutumia miundobinu ya Chuo cha
Mipango ya Maendeleo Vijijini mkoani Dodoma.
Chuo
cha Usimamizi wa Fedha IFM kilianzishwa mwaka 1972 kikianza na kozi
mbili na kutoa wanafunzi 75 lakini hivi sasa chuo hicho kinatoa kozi 23
ambapo mwaka huu wahitimu 2692 wamemaliza masomo yao.