Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia (Pichani Juu) amepokea
kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Songea
Mjini (CCM), Leonidas Gama.
Kutokana na msiba huo, Rais Karia ametua salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Kadhalika
Rais Karia ametuma salamu za salamu rambirambi kwa Mwenyekiti wa Chama
cha Mpira wa Miguu Ruvuma (FARU), Golden Sanga pamoja na Mwenyekiti wa
Majimaji ya Songea, Steven Ngonyani na wanafamilia wote wa mpira wa
miguu na wananchi wote wa mjini Songea.
“Songea
ina historia ya mpira na akina Gama ni chachu ya maendeleo ya mpira wa
miguu Songea. Tumepoteza hazina nyingine, lakini niombe tu familia ya
Gama, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa subira katika kipindi
hiki kigumu kwao,” amesema.
“Nawapa
pole nyingi sana na kupitia viongozi wa FARU, Majimaji, Mlale JKT na
wanafamilia wengine wa soka katika Mkoa wa Ruvuma, naomba mfikishe
salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu,” amesema Rais Karia.
Rais
Karia amesema anamkumbuka Gama kwa uhodari wake katika nyadhifa
mbalimbali za uongozi ikiwemo ukuu wa wilaya, mkoa na ubunge kwani
alifanya kazi kwa kujiamini na kupenda kupigania maendeleo hususani
mpira wa miguu bila kuchoka.