Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), iliyokutana Novemba 22, 2017, katika ofisi za TFF
Karume, pamoja na mambo mengine ilijadili shauri la mapingamizi
mbalimbali yaliyowekwa na timu za Ligi ya Wanawake.
Timu
ya Mburahati Queens iliweka pingamizi kwa mchezaji Ever Kombo ikipinga
timu ya Baobab kumtumia kwa kuwa hakulipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu
wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake.
Kamati imeiruhusu timu ya Baobab kumtumia mchezaji huyo baada ya Mburahati Queens kuondoa pingamizi hilo.
Aidha
Kamati imeiruhusu timu ya Fair Play ya Tanga kumtumia mchezaji
Anastazia Mmwacha baada ya timu ya Mburahati Queens kuondoa pingamizi
iliyomuwekea kwa kutolipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52
toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake.
Kamati
imeiruhusu timu ya Panama kumtumia mchezaji Sabina Mbuta aliyewekewa
pingamizi na Mburahati Queens kwa kutolipiwa ada ya uhamisho kwa mujibu
wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake,Panama wameruhusiwa
kumtumia baada ya kulipa ada hiyo ya shilingi laki moja(100,000).
Timu
ya Marsh Academy imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Asfaty Kasindo,Janeth
Simba ,Rose Mpoma na Arafa Ramadhan wa Mlandizi Queens,Monica
Conrad,Christer J Bahera na Niwael Makuluta wa Mburahati Queens, Neema
Kiniga wa Kigoma Sisters baada ya kukubali kuzilipa timu zao ada ya
uhamisho kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya Wanawake na
timu hizo kukubali kuondoa pingamizi.
Nayo,
timu ya JKT Queens imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Najiat Abassi,Fumu
Ally,Hamisa Athuman wa Ever Green Queens,Fatuma Makusanya na Elizabeth
Kadonya wa Mburahati Queens baada ya timu zao kuondoa mapingamizi
waliyoweka kwa wachezaji hao kutolipiwa ada ya uhamisho.
Timu
ya Simba Queens imezuiwa kuwatumia wachezaji Zainab Rashid wa Ever
Green Queens, Grace T Mbelayi, Jackline Kulsanga, Dinna Omary wa
Mlandizi Queens, na Halima Hamdani Mchen wa Kigoma Sisters mpaka pale
watakapolipa ada ya uhamisho wa shilingi laki moja (100,000) kwa kila
mchezaji kwa mujibu wa kanuni ya 52 toleo la 2017 ya ligi ya wanawake.
Mapingamizi
yaliyowekwa na timu ya Makongo High School kwa timu mbalimbali ikipinga
timu hizo kuwatumia wachezaji wake bila kulipa ada,mapingamizi hayo
yametupwa baada ya timu hiyo kushindwa kufika kutetea hoja za
mapingamizi hayo.
Timu
ya Marsh Academy ya Mwanza imeruhusiwa kuwatumia wachezaji Zainab
Hassan Kienje na Silva Daud waliowekewa pingamizi na timu ya Kigoma
Sisters ambayo ilishindwa kufika kwenye kikao cha kujadili pingamizi
lake.
Wachezaji
Asia Juma,Betista Othuman Abdala na Josephine Julius Nyirenda
wameruhusiwa kucheza timu ya Baobab baada ya timu ya Kigoma Sisters
iliyowawekea pingamizi kuamua kuyaondoa mapingamizi hayo.