Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Wakati
mchezo wa TFF ikisimamisha mchezo wa Azam Sports Federation Cup kati ya
Forodhani FC ya Mara na Ambassodor ya Kahama, Mchezo wa Bulyanhulu na
Area C, sasa utafanyika kesho Jumatano Novemba 8, mwaka huu kwenye
Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Mchezo kati ya Forodhani FC ya Mara na Ambassodor ya Kahama,
umesimamishwa kusubiri uamuzi wa Kamati ya Mashindano baada ya Baruti
ambayo imelete malalamiko kuhusu nafasi yake.
Michezo mingine inayochezwa leo Jumanne ni Msange na Mirambo kwenye
Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi; Pepsi na Kilimanjaro Heroes kwenye Uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga; Mji Mkuu na Nyundo kwenye Uwanja wa Mpwapwa
mkoani Dodoma.
Eleven Stars itacheza na Ndovu kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani
Kagera, Changanyikeni itacheza na Reha Uwanja wa Bandari, Dar es Salaam
wakati Bodaboda itacheza na Kitayosce Uwanja wa Nyerere, Mbulu mkoani
Manyara.
Mbali ya mchezo kati ya Bulyanhulu na Area C, mechi nyingine za kesho
Jumatano, Novemba 8 zitakuwa ni kati ya Cosmopolitan na Abajalo kwenye
Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati makumba Rangers watacheza na
Green Warriors kwenye Uwanja wa Bandari, Dar es Salaam.
AFC ya Arusha itaikaribisha Nyanza FC kwenye Uwanja wa Ushirika; Boma
Fc na African Sports watacheza kwenye Uwanja wa Ushirika; huku
Motochini ikicheza na Ihefu wakati Stand Misuna watacheza na Madini
ilihali Burkina FC itaialika Mbinga United kadhalika Mkamba Rangers
itacheza na Makambako FC kwenye Uwanja wa Sabasaba.
EmoticonEmoticon