UNAFAHAMU KWAMBA UNAWEZA KUAGIZA CHAKULA UKIWA HAPO ULIPO?

November 08, 2017
Na Jumia Food Tanzania

Katika maisha ya sasa yenye pilikapilika takribani siku nzima, muda umekuwa ni bidhaa adimu na kitu ambacho kinazingatiwa sana. Si jambo la kushangaza kujikuta unapitiwa mpaka kufika saa kumi za jioni haujatia kitu chochote tumboni huku muda ukiwa hauko upande wako tena.

Lazima tukubaliane na uhalisia kwamba kuna wakati muda unakuwa sio rafiki ili kuendana na majukumu tuliyonayo, ukizingatia wengi wetu tukifanya kazi kwa waajiriwa ambao hutulipa kulingana na muda tunaotumia kazini. Ili kukabiliana na changamoto kama hii unahitaji mbadala wa kukufanya uendelee na shughuli zako za siku bila ya kuhofia kupoteza muda na kuhatarisha kazi yako.

Kutokana na maendeleo ya tekinolojia duniani hususani mtandao wa intaneti, hivi sasa kuna mfumo unaokuwezesha ukaagiza chakula na kukufikia papo hapo ulipo. Hii inamaanisha kwamba kama vile unavyokwenda kwenye mgahawa unaoupenda au kuuzoea, ukatazama orodha ya vyakula vilivyopo, bei zake na kuagiza chakula ukipendacho ndivyo Jumia Food inavyofanya.

Ikiwa na orodha ya takribani migahawa 70 tofauti yenye aina ya vyakula mbalimbali jijini Dar es Salaam, Jumia Food inawakutanisha wateja na watoa huduma kwa kuwarahisishia kuagiza chakula kwa urahisi na kuwafikia ndani ya muda mfupi popote pale walipo. Mtu anaweza kuwa anajiuliza kwamba atakuwa na uhakika gani kuwa chakula atachokiagiza kitakuja kama vile alivyotarajia?
Jibu ni rahisi. Tunafahamu kwamba kwa watanzania walio wengi bado ni wageni na huduma za mitandaoni kwa sababu huwa tunapenda kufanya maamuzi ya kufanya manunuzi juu ya bidhaa fulani mpaka tuione, kuigusa pengine kuijaribu. Lakini linapokuja suala la chakula watu wengi huwa wanafahamu mahali wanapopendelea kula, chakula wanachokipendelea, ladha pamoja na bei yake.

Hivyo basi kama mtu unakuwa unafahamu chakula ukipendacho kinapatikana mgahawa fulani kwanini usiagize na ukaletewa pale ulipo?
Sio kila siku utakuwa na muda wa kutosha wa kukufanya ukatoka kazini na kwenda nje kula. Na haimaanishi kwamba ukikosa muda wa kutoka nje basi ndio usipate fursa ya kula. Jumia Food imeliona hilo na kwa muda mrefu sasa na kuamua kuja na mfumo ambao utakuwa ni msaada kwako huku wewe ukiendelea na shughuli zako.

Kwa hiyo kama upo kazini na unafahamu kwamba umetingwa na kazi ambazo zinaweza kukupelekea ukakosa muda wa kwenda kupata chakula usiwaze. Kwa sababu unaweza ukatenga muda mfupi, nusu saa au saa moja kabla, kwa kuingia kwenye mtandao wao aidha kwa njia ya kompyuta, tabiti au simu yako ya mkononi na kuagiza chakula ukipendacho kutoka kwa mgahawa uupendao kisha ukaendelea na shughuli zako.

Kwa mfano, unaweza kuwa upo ofisini maeneo ya Posta, umetingwa na kazi au mvua imenyesha na muda wa kupata chakula cha mchana unakaribia na haufahamu utatoka vipi. Cha kufanya ni rahisi, ingia kwenye tovuti yao na kisha weka eneo ulilopo na kisha utaona migahawa yote iliyokaribu nawe inajitokeza kama vile Marrybrown au Rhapsody’s.

Lakini pia mfumo huu unakupatia fursa ya kujaribu vyakula vingine tofauti kutoka kwenye migahawa tofuati iliyo karibu nawe. Kwani unao uwezo wa kuperuzi kwenye tovuti na kujionea vyakula vilivyopo na gharama zao badala ya kutembelea mmoja baada ya mwingine au kwenda kula bila ya kujua gharama zao.
Mbali na mfumo huu kuwa na faida kubwa kwa wateja lakini pia una manufaa kwa wamiliki wa migahawa pia. Kupitia mfumo huu wamiliki wa migahawa hujipatia idadi kubwa ya wateja kutoka kila mahali ambao sio lazima wafike pale moja kwa moja. Hivyo basi kama mgahawa unatoa huduma ya vyakula vitamu na hauna sehemu ya kutosha kuwahudumia wote basi inaweza kuwafikishia chakula popote walipo. Ni rahisi kujiunga na haigharimu gharama yoyote.

Katika zama tulizopo sasa ambapo wengi wetu tunalipwa kulingana na muda tunaotumia kufanya kazi hatuna budi kuwa makini sana. Makampuni na taasisi nyingi hutoa muda wa saa moja kwa wafanyakazi wao kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Muda huo kama ukiugawa kwa makini kwenda kutafuta chakula, kula chakula, kupumzika kidogo na kisha kurudi kazini, utakugundua kwamba watu wengi hutumia takribani dakika 20 mpaka 30 kula huku zingine zikipotea njiani kwenda na kurudi kufuata chakula.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »