RC APIGA MARUFUKU UTOAJI WA LESENI ZA UCHIMBAJI WA MADINI AMANI MUHEZA

October 18, 2017

MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akizungumza wakati wa uzinduzi wa Jumuiya Tatu za Zigi Juu,Zigi Chini na Kuhuhwi zilizopo kwenye Bonde la Mto Pangani katika eneo Amani wilayani Muheza na mradi wa maji mserereko kwa ajili ya vijiji vya Mashewa,Kimbo na Shembekeza

 MKUU wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
 MKUU wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza katika uzinduzi huo

Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa  UNDP ambao wamefadhili mradi huo akizuungumza katika uzinduzi huo
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muheza akizungumza katika uzinduzi huo Jumanne Omari
 Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi kushoto akimuelekeza sehemu ambazo mazingira yameharibiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ambaye alitembelea eneo hilo juzi ambalo ni vyanzo vya maji limekuwa likitumiwa na wachimbaji wa madini ambapo serikali imetaka leseni zilizotolewa zifutwe
 Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi kushoto akimuelekeza sehemu ambazo mazingira yameharibiwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ambaye alitembelea eneo hilo juzi ambalo ni vyanzo vya maji limekuwa likitumiwa na wachimbaji wa madini ambapo serikali imetaka leseni zilizotolewa zifutwe
 Baadhi ya maeneo yaliyoathirika kutokana na uchimbaji haramu wa madini katika eneo la Hifadhi ya Amani wilayani Muheza
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akitembelea maeneo hayo kujionea athari ambazo zimetokana na uchimbaji haramu wa madini kwenye eneo la vyanzo vya Maji Amani na Hifadhi ya Msitu
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jumuiya ya watumiaji wa Maji na Mradi wa Maji Mserereko kwa vijiji vya Masheww,Kimbo na Shembekeza wilayani Muheza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella katikati akizundua mradi huo kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo anayeshuhudia mwenye kilembe cheusi kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Mhandisi Zena Saidi
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akimtwisha ndoo mkazi wa eneo hilo kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa kwanza kulia ni Kaimu  Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga,Mhandisi Laurian Rwebembeza kushoto  ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabriel
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Said

Sehemu za wananchi wakishuhudia uzinduzi huo
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martini Shigella ameitaka wizara ya Madini kuacha kuendelea kutoa leseni za uchimbaji wa madini eneo hifadhi ya Amani wilayani Muheza huku wakitaka zilizotolewa kufutwa kutokana na uharibifu wa mazingira unaoendelea kwenye eneo hilo.

Kwani uchimbaji huo umekuwa na madhara makubwa kuharibu mazingira kutokana na kutumia kemikali  ambazo huingia kwenye maji na hivyo kuleta adhari kubwa kwa binadamu ambayo huyatumia kwa matumizi mbalimbali.

Aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Jumuiya za watumiaji maji Bonde Dogo la Mto Zigi katika Uzinduzi wa Jumuiya tatu za Zigi Juu,Zigi Chini na Kihuhwi zilizopo Bonde la Pangani.

Mradi huo wa Maji wa Mserereko ulihusisha vijiji vya Mashewa,Kimbo na Shembekeza wilayani Muheza Mkoani Tanga.

Alisema pia licha ya kupiga marufuku hiyo lakini watahakikisha wanawachukulia hatua watumishi watakaoshirikiana na wachimbaji kwa kuwakamata na kuwapeleka kwenye vyombo vya dola ili kuweza kukomesha tatizo hilo.

“Labda nisema tu sisi kama mkoa tumepiga marufuku uchimbaji wa madini katika eneo hili la Amani lakini pia tunaitaka Wizara ya Nishati wasiendelea kutoa leseni za madinina mtu atakayekwenda kuchukua leseni hela yake  itakuwa imeibiwa”Alisema  

“Lakini pia niseme pia kwa wale ambao leseni wamepewa zifutwe kwani kuendeleza uchimbaji huo kunaweza kusababisha madhara makubwa sana kwa uharibifu wa mazingira “Alisema.

Alisema iwapo uharibifu huo utaendelea utasababisha hata upatikanaji wa maji kutokuwa mzuri hasa ukizingatia uwepo wa mahitaji muhimu  ya maji kuongezeka kutokana na mradi wa bomba la mafuta watu watashindwa kupata maji.

“Natambua kuwepo kwa wawakilishi kutoka shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa la (UNDP) na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (GEF) ambao wanafadhili mradi wa usimamizi wa pamoja na rasilimali za maji kupitia usimamizi endelevu wa matumizi bora ya ardhi katika mabonde madogo ya mito Ruvu na Zigi”Alisema.

Alisema changamoto za kupungua kwa maji unazidi kuongezeka na kuathiri shughuli za kiuchumi ikiwemo za kijamii hususani za uzalishaji wa chakula,viwanda,umeme na kulinda bayoanuai.

“Upungufu huu huchangia na sababu mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi na shughuli za kibinadamu zinazoongezeka siku hadi siku hasa za uchimbaji wa madini,ukataji ovyo wa misitu “Alisema

Naye Mhifadhi wa Amani,Mwanaidi Kijazi alisema utalii ikolojia umekuwa ukikua kila ambapo kwa mwaka 2007 /2008 watalii walishuka na kufikia 320 na kupanda mpaka mwaka jana 685 ambo ni watalii ambao wana mchango mkubwa kuileta mapato nchi.

Alisema pia kuanzishwa kwa miradi inayo saidia kuzua kasi ya uharibu wa mazingira kwa wananchi kuboresha kipato chao imesaidia kupunguza kwa asilimia kubwa uharibifu wa mazingira.

“Miradi ya ufungaji vipepeo, kilimo cha uyoga ambacho wanashirikiana na Unesco muhoga,karafuu,iliki ufugaji swa samaki,nyuki kwa wadau hao umesaidia kwa asilimia kubwa wananchi waweze kupata kipato “Alisema.
  
Kwa upande wake,Kaimu  Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Tanga,Mhandisi Laurian Rwebembeza amesema hakuna leseni yoyote itakayotolewa kwa wachimbaji wa madini eneo la Amani wilayani Muheza kutokana na maeneo yao kutengwa kwa
ajili ya uhifadhi.

Licha ya hivyo lakini pia wamefuta leseni 14 za wachimbaji wa madini ikiwemo kutoa tahadhari kwa watakaoendelea na zoezi hili kuacha mara moja kabla hawajakumbana na
mkono wa kisheria.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »