Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb) (kushoto) akisalimiana na badhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Mkoani Kagera alipowasili katika Ofisi hiyo ili kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu
Kijaji (Mb) akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani
Kagera kuhusu masuala ya kiutendaji alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani humo.
Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoani Kagera, Bw.
Adam Ntoga, akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Mamlaka hiyo kwa Naibu Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipofanya ziara ya kikazi
katika Ofisi za Mamlaka hiyo Mkoani Kagera.
Baadhi ya Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani
Kagera wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumzia kuhusu uadilifu katika kazi na utoaji
wa elimu kwa mlipakodi baada ya Naibu Waziri huyo kufanya ziara ya kikazi
katika Ofisi hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akizungumza na viongozi
pamoja na watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoani Kagera,
alipofanya ziara ya kikazi katika Mkoa huo ambapo amewaasa kuwa waadilifu
katika kazi zao.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb) (katikati -walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera na baadhi ya Maafisa Waandamizi katika
Mkoa huo.
Mwenyekiti
wa Wafanyabiashara Mkoa wa Kagera Bw. Seif Mkude
(kulia) akielezea kuhusu utayari wa wafanyabiashara wa Mkoa huo kulipa
kodi
wakati wa Mkutano kati ya wafanyabiashara wa Mkoa huo na Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati).
Mfanyabiashara wa Mkoa wa Kagera Bw. Taimur Manyilizo, akieleza
changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wafanyabiashara Mkoani humo ikiwemo kile
alichoeleza uwepo wa taasisi nyingi
zinazodai kodi nyingi ikiwemo OSHA, TFDA, Zimamoto ambapo aliiomba Serikali
iziangalie na kuzifanyia kazi
Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akizungumza kuhusu
ushirikiano kati ya Serikali na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Kagera katika kukuza
Uchumi wa nchi baada ya Naibu Waziri huyo kufanyaziara ya kikazi Mkoani humo.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - WFM)
Benny Mwaipaja, KAGERA
Serikali
imelipa madeni ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi
yanayofikia kiasi cha shilingi bilioni 190 katika kipindi cha miezi
mitatu kuanzia Julai hadi Septemba mwaka huu baada ya kufanya uhakiki wa
madeni halali inayodaiwa na wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali.
Hayo
yamesemwa Mjini Bukoba mkoani Kagera na Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe. Dokta Ashatu Kijaji (Mb), wakati akizungumza na Jumuiya ya
Wafanyabiashara wa mkoa huo akiwa katika ziara ya kikazi kukagua
utendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Huduma ya
Ununuzi Serikalini (GPSA).
Dokta
Kijaji alisema kuwa wazabuni wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 67.2,
wakandarasi wamelipwa shilingi bililioni 24.2, watoa huduma mbalimbali
wamelipwa Shilingi bilioni 38, watumishi wa umma wamelipwa Shilingi
bilioni 37, huku wadai wengine wakilipwa shilingi bilioni 24.
Alisema
kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017, Serikali imetenga zaidi ya
Shilingi trilioni 1 kwa ajili ya kulipa madeni mbalimbali na kwamba
itaendelea kulipa madeni yote yaliyohakikiwa.
Dkt.
Kijaji aliiambia Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera kwamba
Serikali inatambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya Taifa kutokana
na kulipa kodi zinazochangia kuboresha miundombinu na huduma mbalimbali
za jamii.
Alitoa
wito kwa wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki katika
biashara zao, kutoa stakabadhi wanapouza bidhaa na huduma huku wananchi
wakiaswa kudai stakabadhi wanapofanya manunuzi ya aina yoyote na
kuhakikisha kuwa stakabadhi hizo zinaonesha kiasi halisi walicholipia
huduma na bidhaa walizonunua.
Akizungumza
kwaniaba ya Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoani Kagera, Mwenyekiti wa
Jumuiya hiyo Bw. Seif Mkude, alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya
Tano kwa namna inavyohamasisha na kushikia bango masuala ya kodi kwa
manufaa ya Taifa.
Alisema
kuwa wafanyabiashara wameridhika na namna kodi wanazolipa
zinavyosimamiwa kikamilifu na kutekeleza miradi dhahiri ya maendeleo na
kuahidi kuwa wataendelea kulipa kodi hizo ili kujenga uchumi wa nchi.
Alitoa
wito kwa wafanyabiashara wenzake kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili
kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli huku
akiishauri Serikali kuondoa kero ndogondogo zilizotolewa na
wafanyabiashara wakati wa mkutano huo.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Kagera, Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bw.
Deodatus Kinawiro, aliwashauri wafanyabiashara hao kupanua wigo wa
biashara zao ili waweze kunufaika na uwepo wa soko huru katika nchi
zaidi ya nne zinazopakana na mkoa huo ikiwemo Uganda, Rwanda, Burundi,
DRC Kongo, Kenya na nchi nyingine.
Alisisitiza
umuhimu wa wafanyabiashara hao kusafirisha bidhaa zaidi nje ya nchi ili kuvutia
fedha za kigeni.
EmoticonEmoticon