Kundi la watayarishaji wa muziki
na Madj maarufu wa Marekani, Major Lazer limeachia video ya wimbo wao “Particula”
iliyofanyika katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini na kuongozwa na mtayarishaji wa
filamu, Adriaan Louw.
Kwenye video hii yenye muonekano wa Kiafrika, wanaonekana mastaa
wa Afrika Kusini, Dj Maphorisa na Nasty C, rapper wa Nigeria Ice Prince, na
msanii wa Marekani mwenye asili ya Nigeria, Jidenna.
“Particula” inapatikana kwenye EP mpya ya Major
Lazer iitwayo Know No Better ambayo waliichia kwa kushtukiza mapema mwaka huu
na kupokelewa kwa sifa nyingi.
Nyimbo zinazopatikana kwenye EP
hiyo zimetazamwa kwa kiasi kikubwa mtandaoni ambapo wimbo uitwao “Sua Cara” waliowashirikisha
mastaa wa Brazil, Anitta na Pabllo Vittar ni moja ya video zilizotazamwa
zaidi Youtube kwa zaidi ya mara milioni 217 hadi sasa.
EP hiyo imekusanya ladha za dunia
nzima na imeshawishiwa na safari yao huko Pakistan, Cuba, America Kusini na
Afrika huku wakiongezea ladha za Carribean.
Know No Better imekusanya wasanii mashuhuri
kuanzia Machel Montano, Busy Signal, Sean Paul, Konshens, J Balvin na wengine
huku watayarishaji kama Jr. Blender, Boaz van de Beatz na King Henry wakihusika
pia.
Know No Better inafuata mafanikio
ya ngoma za Major Lazer zikiwemo “Run Up” waliowashirikisha PARTYNEXTDOOR na Nicki
Minaj, “Cold Water” waliowashirikisha Justin Bieber na MØ pamoja na “Lean On” wakiwa
na DJ Snake na kumshirikisha MØ, ambao umekuwa moja ya nyimbo zilizofanikiwa
katika muda wote.
Major Lazer kwa sasa wanafanya
ziara dunia nzima.
Fuata Link hii kuitazama video ya
Particular https://youtu.be/CtEHrcA8dKc
EmoticonEmoticon