Waziri wa
Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akiongea na Baadhi wa wafugaji na Viongozi wa
Mkoa wa Kilimanjaro hawapo katika Picha, alipofanya ziara ya dharula katika
kijiji cha Kyara wilayani Mwanga ambapo umetokea uingizwaji wa mifugo kinyume
cha sheria na wafugaji wanaosadikika kutoka nchi jirani ya Kenya.
Katika Picha
Waziri Mpina akiwa katika kikao na uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro alipofana
ziara ya Dharula. Baada kuwepo kwa uvamizi wa mifugo kutoka Kenya.
Waziri wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina kushoto na Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo sekta ya Mifugo Dkt Maria Mashingo walipokuwa katika kikao na uongozi wa
mkoa wa Kilimanjaro.
NA MWANDISHI MAALUM
-MWANGA
Ikiwa ni siku ya nne baada ya kupewa dhamana ya kuongoza
Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli, Waziri Luhaga Mpina amefanya ziara ya dharula katika
Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo, na kuagiza uongozi wa Mkoa huo kupitia
mwanasheria wa serikali wa mkoa, ndani ya siku saba kuzipiga mnada ng’ombe zote
zilizoingizwa katika kijiji cha Kyerwa kinyume na sheria na taratibu za nchi.
Mpina ameagiza Idadi ya Ng’ombe hao 1325 kupigwa mnada katika zoezi ambalo
litasimamiwa na mwanasheria wa serikali, na kusema kuwa vyombo vya dola viendee
kuhakikisha kuwa hakuna ng’ombe atakayepita wala kutoroshwa katika hali yoyote
ile.
Aidha Mpina amevitaka vyombo vya dola kuendelea kuwasaka
ng’ombe zaidi ya 4000 wanaosadikiwa kutoroshwa na kuwakama pamoja na kuchukua
hatua stahiki, na amemtaka mhifadhi mkuu (TANAPA) asaidie kutoa vifaa ikiwa ni
pamoja na helicopter na drown ili kuweza kusaidia oparesheni za kusaka mifugo
iliyotoroshwa na mingine inayoendelea kuingia kinyemela nchini.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira,
alieleza kuwa uvamizi huo wa Mifugo unasababisha tishio la kuambukizwa kwa magonjwa kwa mifuko ambayo mkoa inayo
pamoja na uharibifu wa mazingira hali inayopelekea mkoa kushindwa kufikia
malengo ya kujitengea maeneo ya ufugaji, pamoja, uhaba mkubwa wa malisho na
uhaba wa maziwa ambapo mwanga pekee ina ng’ombe zaidi ya 18,000.
Akiongea katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kutoka
sekta ya Mifugo Dkt Maria Mashingo alisema kwa kuwa ng’ombe hao wanatakiwa
kuchukuliwa vipimo ili kujua kama wameathirika na magonjwa ya mifugo kwa na aliafiki
wazo la kuteketeza kabisa ng’ombe hao endapo watapatikana na magonjwa
yasiyotibika.
Madhara mengine yaliyoelezwa kutokana na uvamizi wa mifugo
hiyo ni pamoja na uharibifu wa vyanzo vya maji, misitu na ongozeko la migogoro
kati ya wakulima na wafugaji.
EmoticonEmoticon