BENKI YA CRDB YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA WILAYANI CHATO

October 07, 2017

Na Binagi Media Group
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja mwaka huu 2017, benki ya CRDB jana simetoa semina kwa wateja wake katika wilaya ya Chato mkoani Geita na pia kupokea maoni yao ili kuboresha zaidi huduma zake.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini aliwahakikishia wateja wa benki hiyo huduma ya mikopo kwa muda wa siku saba na hivyo kuwahimiza wafanyabiashara kuitumia benki fursa hiyo kukuza mitaji yao ya biashara.

Aidha alisisitiza kwamba benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake ikiwa ni benki inayoongoza kwa kutoa mikopo hapa nchini huku pia jamii ikiendelea kunufaika na benki hiyo kupitia gawio la faida ambalo hutolewa kila mwaka ili kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo afya na elimu.

“Tunaomba tuendelee kushirikiana pamoja ambapo CRDB ni benki ya muda mrefu iliyo salama na imara kufanya nayo kazi ikiongoza kwa zaidi ya miaka 10 sasa kwa kutoa huduma bora na zenye riba nafuu nchini”. Alisisitiza Nkini kwenye semina hiyo iliyojumuisha pia wateja wa CRDB kutoka Geita, Muleba, Ngara na Bihalamulo.

Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga alisema benki hiyo imeendelea kuwafikia wateja wake kote nchini kupitia huduma mbalimbali ikiwemo Fahari Huduma, Simu Banking pamoja na Internet Banking na hivyo kuwa benki yenye mtandao mkubwa unaowawezesha wateja wake kupata huduma za kibenki popote walipo.

“Huduma zetu ni bora kuliko benki nyingine yoyote nchini hivyo natoa rai wateja wetu kutumia huduma zetu ikiwemo mikopo kwa ajili ya mitaji ya biashara zao kwani tunao uwezo mkubwa wa kuwahudumia”. Alidokeza Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus.

Baadhi ya wateja wa CRDB, Mellia Alloyce pamoja na Ristides Ramadhan walikiri kunufaika na benki hiyo kupitia huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya mikopo na hivyo kukuza biashara zao huku hivi sasa wakifurahia uharaka wa huduma hiyo tofauti na hapo awali.

Katika hatua nyingine benki ya CRDB ilisaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi za Kalema, Muungano na Katemwa A katika halmashauri ya wilaya ya Chato ambapo msaada huo ulijumuisha mifuko 150 ya saruji, mabati, sinki za vyoo pamoja na vyombo vya kukusanyia taka na tenki la maji kwa ajili ya halmashauri hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas aliishukuru benki hiyo na kubainisha kwamba bado kuna uhaba wa vyoo kwenye shule nyingi na kuiomba kuendelea kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo ili kutoa chachu kwa wadau na benki nyingine kuiga mfano huo. Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodlack Nkini, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji CRDB. Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye semina hiyo. Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga akizungumza kwenye semina hiyo. 
        Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas , akichangia mada kwenye semina hiyo.        

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »