Kampuni ya Ulinzi ya SGA imezindua chata mpya ya huduma kwa wateja ikiwa ni sehemu ya maadhinisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Akizindua
chata hiyo mpya, Mkurugenzi Mtendagi wa SGA Tanzania, Eric Sambu
alisema kampuni hiyo inaweka mikakati madhubuti ili kuendana na matakwa
na mahitaji ya wateja wao hasa katika mazingira ya sasa ya biashara
ambayo yanabadilika kila kukicha.
Alisema
kuna mabadiliko mengi mno katika soko na hivi kulazimu makampunni mengi
kufanya mabadiliko ili kuendanana na hali halisi na makampuni mengi
bado hayajaweza kusimama imara.
“Ili
kuendana na hali halisi ya sasa hivi ni lazima tuendane na mazingira
yalivyo ili tuweze kutoa huduma nzuri kwa wateja wetu,” alisema Bw. Sambu.
Alisema
SGA inaadimisha miaka 33 nchini Tanzania huku ikiwa imepata mafanikio
mazuri hasa katika miaka mitano iliyopita na kusisitiza kuwa wameweza
kupata mafanikio haya kutokana na kuboresha utendaji kazi, kuwezesha
wafanyakazi kupitia mafunzo mbalimbali katika vitengo vyote. Kwa mujibu
wa Mkurugenzi Mtendaji huyo, chata hii mpya inamlenga mteja zaidi katika
utendaji wa SGA.
“Mabadiliko
ya hivi karibuni katika ufanyaji biashara Tanzania yametupa fundisho
kubwa na nafasi ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wetu wote katika ngazi
zote ili waweze kuwahudumia wateja vizuri zaidi na kukidhi matakwa mapya
ya soko sasa hivi na hili kwetu sasa hivi limekuwa jambo la kawaida,”
“Tunaendelea
kuboresha mifumo yetu na kuwekeza zaidi katika teknolojia na rasilimali
watu ili kuhakikisha tunafanya vizuri. Tumeweza kuhakikisha tunapata
hati safi katika usimamizi wa ubora tangu mwaka 2001 (ISO certification
on Quality Management System) na hivi karibuni tumepata hati safi ya
afya na usalama (Occupational Health and Safety ISO 18001 Standard).
Meneja
wa Uhusiano wa Wateja wa SGA, Aikande Makere, alisema wanaamini chata
hii mpya itahakikisha kuwa wateja na wadau wote wanapokea huduma
wanayostahili kwa kiwango cha juu kwa kuzingatia uaminifu, uwajibikaji,
usawa na wepesi wa kubadilika kulingana na mazingira.
“Tunawashukuru wateja wetu wote ambao wamekuwa pamoja nasi hata katika kipindi hiki chenye changamoto kubwa katika biashara,” alisema Aikande.
SGA
ndio kampuni kongwe ya binafsi ya ulinzi nchini Tanzania huku ikiwa
imeajiri zaidi ya watanzania 5100 katika maeneo ambayo wanafanya
biashara Tanzania. Wanatoa huduma mbalimbali ikiwemo ulinzi kwa kutumia
maaskari, ulinzi kwa kutumia umeme, huduma za dharura (emergency
response), ufuatiliaji (tracking), usafirishaji wa mizigo na vifurushi
(courier) na usafirishaji wa fedha.
“Tuna
magari 222 na vituo 12 nchi nzima ambavyo vina mitambo ya kisasa na
wafanyakazi waliobobea katika masuala ya ulinzi na tumehakikisha kuwa
tuna miundombinu madhubuti ya kuwahudumia wateja wetu nchi nzima.,” alisema Sambu.
EmoticonEmoticon