Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, amepokea
kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya wanafamilia
wawili wa soka vilivyotokea Oktoba 5, 2017 kwa nyakati tofauti.
Taarifa
ambazo TFF imezipata zinasema waliofariki dunia siku hiyo ni aliyekuwa
Mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’; Zanzibar ‘Zanzibar
Heroes’; pamoja na Afrika Mashariki miaka ya 1950 na 1960, Abdul Majham
na Mwamuzi wa Daraja la Kwanza anayechezesha Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, Mirambo Tshikungu.
“Hakika
nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo hivi. Ni mshtuko
mkubwa sana katika familia ya mpira wa miguu hapa Tanzania, natambua pia
ni majonzi makubwa kwa familia za marehemu,” amesema Rais Karia.
“Niombe
tu kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, majirani kuwa watulivu katika
kipindi hiki cha msiba. Wawe na moyo wa subira baada ya ndugu zetu
kutanguliwa mbele ya haki. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Rehema,
basi na tumuombe awe na msamaha kwa ndugu zetu,” amesema.
Abdul
Majham aliyefariki dunia huko Visiwani Zanzibar ni Mchezaji huyo wa
zamani wa Klabu ya Vikokotoni ya visiwani Zanzibar, pia aliyepata
kuichezea klabu Bingwa ya kwanza ya Tanzania, Cosmopolitan ya Dar es
Salaam.
Kuhusu
Tshikungu, TFF imepokea taarifa inayosema kwamba alifariki dunia jioni
ya Oktoba, 2017 katika Hospitali ya Ikonda iliyoko Wilaya ya Makete
mkoani Njombe alikokuwa akitibiwa.
Mwenendo
wa uchezeshaji wake ulikuwa na tija kwani rekodi zinaonesha kwamba
mchezo wake mkubwa kuuchezesha msimu uliopita ulikuwa ni kati ya
Majimaji ya Songea na Young Africans ya Dar es Salaam uliofanyika Uwanja
wa Majimaji mkoani Ruvuma.
EmoticonEmoticon