KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga |
KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akizungumza wakati wa ufungaji wa baraza kuu la 47 la wafanyakazi mjini Tanga
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi akizungumza katika mkutano huo |
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi kushoto akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka wakati wa kikao hicho |
Mwenyekiti wa Tuico Tanzania,Paul Sangeze akizungumza katika mkutano huo |
Daktari wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya Afya kwa wajumbe wa baraza hilo |
Mmmoja wa wafanyakazi na mjumbe wa baraza hilo akichangia kwenye mkutano huo |
mmoja wa wajumbe wa baraza hilo Janet Vesso akichangia mada |
Wajumbe wa Baraza hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi wa pili kutoka kushoto,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo,Dkt Tito Mwinuka kulia na Mwenyekiti wa TUICO Taifa Paul Sangeze wa kwanza kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Wafanyakazi,Asmaa Myale
BARAZA kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco)
limeazimia kuunga mkono jitihada za Rais Dkt John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa
nchi ya watu wenye kipato cha kati kwa kufanya kazi kwa umahiri,uzalendo na
ufanisi.
Akizungumza katika ufungaji wa baraza hilo mwishoni mwa wiki
mjini Tanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,Dr.Alexander Kyaruzi alisema
bodi hiyo ipo tayari kutoa ushirikiano katika kuhakikisha shirika linafikia malengo
yake muhimu.
Alisema malengo hayo ambayo yanahitajika katika kuhakikisha uchumi
wa viwanda unafikiwa kwa kasi kubwa kutakapotokana na kuwa na umeme wa uhakika
ambao unaweza kusukuma gurudumu la maendeleo.
Aidha alisisitiza juu ya umuhimu wa utunzaji wa miundombinu ya
shirika hilo ili iweze kusaidia kutoa huduma zake wakati wote bila kuwepo kwa
vikwazo vya namna yoyote ile.
Hata hivyo aliwaasa wafanyakazi wa shirika hilo kuhakikisha
wanakuwa walinzi wa miundombinu hiyo ili isiweze kuibiwa ikiwemo kuhakikisha
haihujumiwi na watu wanaoweza kufanya hivyo.
EmoticonEmoticon