NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO
wa Pensheni wa PSPF, umezindua ofisi
mpya mbili moja kisiwani Pemba na nyingine kisiwa cha Ukerewe mkoani
Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017,
Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Mfuko huo, Bi. Laila Maghimbi alisema, ofisi
hizo zimezinduliwa rasmi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa
Wateja.
“Mtakumbuka
kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba kila mwaka, huadhimishwa wiki ya huduma
kwa wateja
duniani, na kwa mwaka huu, Mfuko umzindua ofisi mpya kule Pemba na Ukerewe ili
kuboresha zaidi huduma zetu.”
Akizungumzia
mtandao wa PSPF nchini, Bi. Maghimbi alisema, “PSPF ina ofisi kila makao makuu
ya mkoa Tanzania Bara na Visiwani.”
Bi.
Maghimbi alisema, sambamba na ufunguzi wa ofisi mpya,
hapa
makao makuu mtaona tunaadhimisha kwa kushirikiana na washirika wetu kwenye
utoaji huduma mbalimbali, ili kuwapatia fursa wananchama wetu ya kupata huduma
kutoka taasisi hizo washirika.
Aliwataja
washirika hao ambao wameweka mabanda ya kutoa huduma kuwa ni pamoja na Mfuo wa
Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), benki za TPB, NMB, CRDB na Benki ya Walimu,
(MCB).
Alisema,
PSPF katika maadhimisho hayo, inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kuwahudumia wastaafu wanaofika kujua mafao yao, pia kusajili wanachama wapya
kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari yaani PSS.
Miongoni
mwa wanachama wa PSPF waliofika kupatiwa huduma ni pamoja na Mkuu wa Mkoa
Mstaafu, Dkt. Ibrahim Msengi ambaye alisifu huduma za haraka zitolewazo na
maafisa wa PSPF.
“Kwa
kweli mimi nimeridhishwa na huduma niliyopatiwa hapa, nimefika hapa kufuatilia
malipo ya mirathi ya ndugu yetu, na nimepokelewa vizuri na kupatiwa huduma
stahiki bila ya ucheleweshwaji, hili ni jambo jema na niwapongeze PSPF kwa
uchapakazi wa namna hii.” Alisema.
Wanachama
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wakihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa wateja
makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika
kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili
kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Mwanachama
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa kwenye ofisi ya huduma kwa
wateja
makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika
kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili
kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Mwanachama
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akihudumiwa na Bi.Elizabeth Shayo, (kulia), makao makuu
ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Oktoba 2, 2017. Katika
kuadhimisha wiki hiyo, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili
kusogeza karibu huduma kwa wanachama wake.
Elizabeth Shayo, (katikati),
Afisa Huduma kwa wateja wa PSPF, akitoa maelezo kwa Mwanachama
aliyefika kupatiwa huduma.
Afisa
wa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. January Iman
Buretta, (kushoto), akizungumza na wanachama wa Mfuko huo waliofika makao makuu
kupatiwa huduma Oktoba 2, 2017. Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja
iliyoanza jana, PSPF imefungua ofisi nyingine Pemba na Ukerewe ili kusogeza
karibu huduma kwa wanachama wake.
Ntimi Mwakajila, Afisa wa Huduma
kwa njia ya simu, (Call Centre), Mfuko wa PSPF, akiwa
kazini
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bi. Fatma
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa
wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, (mbele), Meneja
Masoko, Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Fatma Elhady, (wapili kulia), na
maafisa wa kitengo cha huduma kwa njia ya simu wakiwahudumia wateja wa
Mfuko kwenye kituo hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa
wateja, Mfuko wa Penshini wa PSPF, Bi. Queen Edward, akizungumza na
mmoja wa wateja waliofika kupatiwa huduma
Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt.
Ibrahim Msengi, (kulia), akipokea nyaraka kutoka kwa Meneja wa
Huduma kwa Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi.
Laila Maghimbi.
Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Dkt.
Ibrahim Msengi, (kushoto), akipatiwa maelezo na Meneja wa Huduma kwa
Wateja, wa Mfuko wa PSPF, Bi. Laima Maghimbi.
--
Khalfan Said
Photojournalist
K-VIS MEDIA
P.o.box 77807
Dar es Salaam, Tanzania
Mobile: +255-784-646-453/+255-653-813-033
Blog: khalfansaid.blogspot.com
EmoticonEmoticon