Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akikata keki kama ishara ya kuzindua wiki ya huduma
kwa mteja katika benki ya CRDB, Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Singida
Elias Tarimo na anayefuata ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akimlisha keki John Patrick mteja wa benki ya CRDB
ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo cha utumishi wa Umma Singida, kama ishara ya
kuzindua wiki ya huduma kwa mteja katika.
Meneja wa Benki ya
CRDB Singida Innocent Arbogast akijiandaa kumlisha keki Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dkt Rehema Nchimbi wakati wa kuzindua wiki ya huduma kwa mteja katika benki
hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP
Debora Magiligimba kabla hajamlisha keki wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma
kwa Mteja katika benki ya CRDB.
Wateja wa Benki ya
CRDB wakiendelea kupatiwa huduma katika benki hiyo, huku wiki ya huduma kwa
mteja inayolenga kuongeza uaminifu kati ya benki na wateja wake, ikiwa
imezinduliwa.
Wateja wa Benki ya
CRDB wakiendelea kupatiwa huduma katika benki hiyo, huku wiki ya huduma kwa
mteja inayolenga kuongeza uaminifu kati ya benki na wateja wake, ikiwa
imezinduliwa.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida Dkt Rehema Nchimbi ameishauri Benki ya CRDB Mkoa wa Singida kuwasiadia
vijana elimu na mikopo ya kutambua na kutumia fursa zilizopo ili waachane na
kauli za kujiita ‘mabomu yanayosubiri kulipuka’.
Dkt Nchimbi ametoa
ushauri huo mapema leo wakati akizindua wiki ya huduma kwa mteja katika benki
ya CRDB tawi la Singida huku akisisitiza benki hiyo kuwa bega kwa bega na Vijana.
“Vijana wetu wasione
fahari kabisa kujiita mabomu yanayosubiri kulipa, Singida tuna fursa nyingi
wasibweteke watumie benki hizi na nyinyi pamoja na benki nyingine jitahidini
kuwashika vijana hawa wakipewa elimu ya ujasiriamali na mikopo wataifikisha
Singida mbali kiuchumi”, amesema Dkt Nchimbi.
Ameongeza kuwa Mkoa
wa Singida umejipanga kuzalisha chakula cha kutosha ili uweze kulisha makao
makuu ya nchi yaani Dodoma hivyo vijana wabadilike na wawe mabomba ya
kusafirishia chakula na bidhaa mbali mbali.
Dkt Nchimbi ameongeza
kuwa huduma za kibenki zinawasaidia watumishi wa umma katika kupanga matumizi
ya pesa kwakuwa isingekuwa mishahara kupitia benki kungekuwa hakuna
kinachosalia katika mishahara yao huku hicho kidogo kinachosalia kinakuwa cha muhimu
sana.
Ameongeza kuwa kuelekea
uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda huduma bora za kibenki ni hakikisho la
safari hiyo kuwa salama na yenyewe uhakika huku benki zikiwa ni mahali panapo waunganishawajasiriamali
wakubwa kwa wadogo.
Ameongeza kuwa benki
ya Crdb inaaminika ndio maana wajasiriamali na watumishi wengi wamekuwa
wakiitumia hivyo na wateja wao pia wajenge tabia ya kuaminika hasa kwa
kurejesha mikopo yao bila usumbufu.
“Watu wengi wamekuwa
wakikopa bila ya kuwa na malengo hivyo kuishia lawama au hukopa kwa mazoea bila
ya kujiandaa nini atafanyia huo mkopo, mteja wa hivyo anaweza kubadilika na
kutokuwa mwaminifu hivyo benki mna jukumu kubwa la kutoa elimu ya kutosha
wateja wenu”, amefafanua Dkt Nchimbi.
Ameeleza kua benki
iendelee kuwaelimisha wajasiriamali na wananchi wengine kuwa kukopa sio aibu na
mtu ambaye anakopesheka hiyo ni heshima hivyo atambue fursa hiyo na kuitumia
vizuri.
Kwa upande wake
Meneja wa Benki ya CRDB Singida Innocent Arbogast ameeleza kuwa benki hiyo inatoa
mikopo kuanzia kwa wajasiriamali wadogo mpaka wakubwa pamoja na kutoa elimu
pamoja na huduma za Sim banking, malkia akaunti na akaunti za watoto.
Arbogast amesema kuwa
wiki ya huduma kwa mteja wataitumia vizuri kwa kuwatembelea wajasiriamali wote
mitaani na kuelezea huduma zao kwakuwa wiki ya huduma kwa mteja ina lenga
kuongeza uaminifu kati ya benki na wateja wao.
Naye Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba amesema benki hiyo imekuwa ikiwasaidia
watumishi ili waweze kutimiza malengo yao huku watumishi wakiwa waaminifu
katika kurejesha mikopo hiyo.
ACP Magiligimba
ametoa mfano wake yeye ambaye ameweza kujenga nyumba kutokana na mkopo wa benki
hiyo hivyo watumishi wengine wasione aibu kukopa ila wawe wamejiwekea malengo
mazuri ya matumizi ya mikopo hiyo.
|
EmoticonEmoticon