Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu akizungumza wakati
akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo
Wilayani humo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu akizungumza wakati
akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo
Wilayani humo Mkoani Singida.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Ikungi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu wakati wa ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja.
Meneja wa Benki ya NMB Wilaya
ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito akizungumza jambo mara baada ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo
Wilayani humo Mkoani Singida.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu akikata keki ishara ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi, Mkoani Singida.
Shilinde Kurwa Kasule ambaye ni
mfanyabiashara akielezea namna alivyonufaika kwa kupata mikopo mbalimbali kutokana na utunzaji wa fedha zake Benki.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu (Mwenye Shati la kitenge), Kushoto kwake ni Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Winfrida Funto wakiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Ikungi wakiongozwa na
Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito.
Meneja wa Benki ya NMB Wilaya ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu (Kulia) akimsikiliza Meneja wa Benki ya NMB Wilaya
ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa Benki hiyo mara baada ya ufunguzi wa wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi.
Na
Mathias Canal, Singida
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne
Mtaturu amewataka wananchi kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyingi majumbani na
badala yake wajenge utamaduni wa kuzipeleka benki ili kuepusha kuhatarisha
usalama wao.
Ametoa kauli hiyo leo Octoba 2, 2017 wakati
akifungua wiki ya Huduma kwa mteja katika Benki ya NMB Tawi la Ikungi lililopo
Wilayani humo Mkoani Singida.
Alisema tabia ya baadhi ya wananchi kuhifadhi
kiasi kikubwa cha fedha majumbani si nzuri kwa sababu wanahatarisha usalama
wao, hivyo ni vyema wakatumia benki hiyo iliyoanzishwa hivi karibuni kwa ajili
ya kutunza fedha zao.
Alisema mbali ya kuhatarisha usalama kwa
utunzaji wa fedha ndani ya nyumba pia kuhifadhia fedha nyingi ndani Ni kosa
kisheria kwani kunasababisha mzunguko wa fedha kuwa mdogo Jambo ambalo
linafifihisha ukuaji wa uchumi.
Katika hatua nyingine Mhe Mtaturu aliupongeza
uongozi wa benki ya NMB kwa kutii maoni ya waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa Desemba 5, 2016 wakati akifungua
tawi la benki ya Biashara ya Uchumi lililopo wilayani Karatu mkoani Arusha la
kupunguza kiasi cha riba wanachokitoza katika mikopo wanayoitoa ili kuwawezesha
wananchi kukopa na kupata tija.
Alisema kuwa kuanzishwa kwa NMB CHAPCHAP
INSTANT ACCOUNT na kupatikana kwa riba ya mpaka asilimia tano kwa wateja Ni
kichocheo Cha muelekeo wa wananchi kupata Huduma laini katika Benki hiyo
ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.
Sambamba na hayo pia Mhe Mtaturu aliushauri
Uongozi wa Benki hiyo kufanya Utafiti katika maeneo ya Wilaya nzima ili kuwa na
namna Bora ya kuwafikia wateja wote ambao bado hawajaanza kunufaika na Huduma
hiyo na Huduma za kibenki ikiwemo uhifadhi wa fedha Hizo.
Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NMB Wilaya
ya Ikungi Ndg Wilbert Mwalusito alisema kuwa wiki ya Huduma kwa mteja
inawarahisishia wateja kutoa maoni yao ili kuwa na namna Bora ya kuboresha
Huduma katika Benki hiyo.
Alisema kuwa Benki hiyo imeanzisha Huduma ya
Akaunti ya CHAP CHAP ambayo itamuwezesha mteja kupata Huduma za kibenki na
Haina kima Cha chini Cha salio kwenye Akaunti Wala makato ya mwezi.
Aliongeza kuwa NMB CHAP CHAP Akaunti Ni
Huduma Bora na nafuu inayomuwezesha mteja kufanya shughuli zake zote za kibenki
papo kwa papo bill shida popote alipo kwa kutumia Simu ya mkononi kupitia
Huduma ya NMB Mobile.
Naye Shilinde Kurwa Kasule ambaye ni
mfanyabiashara na mtumiaji mkubwa wa Huduma za Benki ya NMB aliwasihi wananchi
na wafanyabishara Wilayani Ikungi kutohifadhi fedha ndani badala yake wahifadhi
Benki kwa ajili ya usalama wao na fedha zao.
Shilinde alisema kuwa kuweka fedha benki Ni
njia mojawapo ya wananchi na wafanyabishara kuiaminisha Benki kuwa
wanakopesheka kwani watakuwa wanajua mzunguko wa biashara ya mteja wao.
EmoticonEmoticon