Itashutiwa katika miji ya Berlin, London, Paris, Cape Town na Acapulco, Mexico
Ø Mastaa wakubwa duniani kama Eric Dane wa Lastship ,Gerard Depardieu wa Life of Pie, Thomas Kretschmann wa Avengers Pearl Thusi wa Quantico…kushiriki
NYOTA
ya aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa, Mtanzania
Idris Sultan, inaendelea kung’ara baada ya ‘kupata shavu’ la kushiriki
filamu yenye bajeti ya dola za Kimarekani milioni 17 sawa na zaidi ya
shilingi bilioni 38.
Idris pamoja na Mtanzania mwingine Ernest Napoleon, wataungana na mastaa wakubwa duniani kama Eric Dame, mwigizaji Mmarekani, Gerard Depardieu wa Ufaransa, Thomas Kretschmann wa Ujerumani na wengine wengi kucheza filamu hiyo ya ujambazi wa kimataifa.
Filamu
hiyo itakayojulikana kwa jina la ‘The Blue Mauritius’, inahusu
majambazi watano wa kimataifa ambao wanasafiri kwenda katika jiji la
Cape Town nchini Afrika ya Kusini, kwa ajili ya kuiba vitu mbali mbali
vyenye thamani kubwa duniani.
Idris
na mwenzake Ernest Napoleon, watasafiri kwenda katika jiji la Cape Town
nchini Afrika kusini mapema mwakani kwa ajili ya filamu hii kubwa
kuwahi kuwahusisha Watanzania.
“D
Street inayo furaha kubwa kugeukia vipaji vya waigizaji wa Kiafrika kwa
kuwaunganisha na waigizaji wa kimataifa kama itakavyokuwa kwa ‘The Blue
Mauritius’,” anasema Dexter Davis, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya D
Street Media Group ya Marekani, inayoanda filamu hiyo
Kwa mujibu wa Davis, filamu hiyo itasambazwa siyo tu Marekani, bali pia katika majumba makubwa ya sinema dunia nzima.
“Ernest na Idris watang’ara, tunasubiri kwa hamu kuwaona tena kwenye skrini kubwa wakifanya makubwa,” anasema Davis
Mapema
mwaka huu, wawili hao walicheza filamu iliyojulikana kama ‘Kiumeni’
ambayo pia Ernest alikuwa ni mzalishaji na kushirikiana na Daniel Manege
kuiandika. Filamu hiyo ilishinda katika Tamasha la Timataifa la Filamu
la Zanzibar ambalo Idris na washiriki wenzake walihudhuria
“Ninayo
furaha kubwa kufanya kazi na Idris katika filamu kubwa kama hii ya The
Blue Mauritius. Ni mwaka wa pekee kwa mimi kufanikiwa kufanya kazi na D
Street. D Street inabadilisha upepo kwa Afrika inapokuja kwenye suala la
kutengeneza filamu,” anasema Ernest
Kwa
upande wake Idris anasema, “Nilikutana Dexter Davis kwenye Maonyesho ya
Filamu ya Kimataifa ya Zanzibar mwezi Julai na nilifurahishwa na namna
ambavyo amevutiwa na vipaji kutoka Afrika. Alivutiwa kufanya kazi na
mimi baada ya kuona ushiriki wangu katika filamu ya ‘Ballin; On the
Other side of the World’ na miezi miwili baadaye nilishiriki Katina
filamu moja ya Kimarekani. Filamu hizi mbili zimenifanya niweze kufanya
kazi nchini Marekani jambo ambalo nilitamani sana,”
Filamu hiyo inatarajia kuanza kuzalishwa mwishoni mwa mwezi wa tatu mwaka ujao (2018).
EmoticonEmoticon