Na
Mathias Canal, Kilimanjaro
Wakulima wa mazao
ya jamii ya mikunde hususani maharagwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
Vijijini Mkoani Kilimanjaro wamesifu mbegu bora aina ya Lyamungo 90, Jesca na
Uyole Njano zinazotolewa kwa wakulima na Taasisi ya Kimataifa ya utafiti wa
mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia Mradi wa N2AFRICA.
Mradi huo
unaotekelezwa kwa wakulima 11 katika vijiji sita vya Wilaya hiyo umekuwa na
mafanikio makubwa kwao kutokana na mafunzo waliyopatiwa ya kulima kisasa kwa
kutumia mbegu kidogo na mavuno makubwa pamoja na kutumia mbolea.
Wakulima hao
wanasema awali kabla ya mradi huo walikuwa wanalima kwa kuchanganya zaidi ya
mazao ya aina mbili tofauti katika shamba moja, kutotumia mbolea na kulima
pasipo kufuata njia za kitaalamu jambo ambalo liliwapelekea kupata mazao kidogo
ambayo hayakuwa na ufanisi mkubwa katika kuimarisha uchumi wao.
Wanasema Kupitia
mbinu bora walizojifunza kwa wataalamu kutoka katika Mradi wa N2AFRICA wamebadili
mfumo wa maisha kwani kwa sasa wanapata mazao ya kutosha na kuwafanya kuhamia
katika kilimo chenya tija kwa ajili ya chakula na biashara.
Janeth Godwin
Shao, Achibold Masimba, Mary Mbuya na Fredy Urio wakazi wa kijiji cha Kiruweni
, Elizabeth Paschal,na Ester Mbando wakazi wa kijiji cha Mawanjeni Kata ya
Mwika Kusini wanasema kabla ya Mradi wa N2AFRICA walikuwa wanapanda mazao
shambani badala ya kupanda mbegu jambo lililofifisha upatikanaji wa mazao
mengi.
Waliomba mradi huo
kuongeza zaidi ufanisi baada ya kufanikiwa katika kuwanufaisha wakulima kupitia
zao la maharagwe sasa waongeze mafunzo kwa wakulima ili kutoa mbegu za mazao
mengine kama vile kunde na choroko.
Moja ya malengo
muhimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, ni kuitoa Tanzania katika kundi la
nchi masikini zaidi duniani na kujenga uwezo zaidi wa kiuchumi kupitia
kilimo utakaoifanya iwe miongoni mwa nchi zenye kipato cha kati kimataifa.
Mtaalamu wa Kilimo
katika Kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika Kusini Elizabeth Josiah alisema kwa
sasa Zao la maharagwe linapendwa na wakulima wengi kwa sababu linachukua muda
mfupi kukomaa, halina gharama kubwa katika uzalishaji wake na lina bei nzuri
sokoni karibu nyakati zote hata wakati wa mavuno (yaani msimu wake).
Alisema kuwa Mkulima
anaweza kulima maharagwe kwa matumizi ya chakula nyumbani kwake au kwa biashara
reja reja au kwa jumla.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kata ya Mwika Kusini Wilfred Ngile alisema Urahisi wa kulima maharage na faida zake lukuki ni kivutio kwa watu wengi sana kwa sasa huku akisema kuwa lakini bila kufuata muongozo wa kitaalam ni ndoto kwa mkulima kupata mavuno anayotarajia.
Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kata ya Mwika Kusini Wilfred Ngile alisema Urahisi wa kulima maharage na faida zake lukuki ni kivutio kwa watu wengi sana kwa sasa huku akisema kuwa lakini bila kufuata muongozo wa kitaalam ni ndoto kwa mkulima kupata mavuno anayotarajia.
Alisema mafanikio
wanayoyapata wakulima sio ya wataalamu bali ni mafanikio yao wenyewe kutokana
na kutumia njia bora kutokana na maelekezo wanayoyapata kutoka kwa wataalamu.
Aidha, aliongeza kuwa
mafanikio hayo yanatokana na Mbegu bora zilizofanyiwa tafiti na Taasisi ya
Kimataifa ya utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiko (IITA) na kutambulika
kisheria ambazo ni pamoja na Uyole Njano, Lyamungu 90, na Jesca.
Naye Afisa Mazao wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini Bi Joyce Kessy
alizitaja changamoto zinazowakabili wakulima kuwa ni pamoja na uzalishaji mdogo
kwani wanazalisha chini ya tani moja kwa hekta ambapo unachangiwa na sababu za
kurudia mbegu, kutotumia mbegu za viwandani, kupanda bila kuacha nafasi, na
kupanda zao moja kwa kuchanganya na mazao mengine.
Hata hivyo alisema kuwa mara baada ya Mradi wa N2AFRICA kuanzishwa katika
Wilaya ya Moshi Vijijini hamasa imekuwa kubwa kwa wananchi kuhitaji mbegu na
mbolea kutoka taasisi ya IIAT hivyo ameiomba taasisi hiyo kuongeza utoaji wa
mbegu kwa wakulima wote na kutoa mafunzo.
Alisema kuwa mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha sekta ya kilimo nchini Tanzania jambo ambalo
limerahisisha utendaji wa serikali kupitia Wizara ya Kilimo.
Alisema kuwa wakulima wanajifunza zaidi kwa vitendo kuliko nadharia hivyo
aliiomba Taasisi hiyo ya IITA kupitia Mradi wa N2AFRICA kuvifikia vijiji vyote
na kuwanufaisha wananchi kwa mafunzo ya vitendo zaidi.
Katika awamu ya kwanza ya Mradi huu ilianzishwa mwaka 2009 na kutekelezwa
katika nchini DR Congo, Ghana, Kenya, Liberia, Malawi, Nigeria, Rwanda, Sierra
Leone na Zimbabwe ambapo Awamu ya pili
ilianza Januari 2014 na kufanyika katika nchi tano za Ethiopia, Ghana, Nigeria,
Tanzania, na Uganda.
Janeth Godwin mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia mradi wa N2AFRICA
Wakulima wa zao la maharagwe walipowapokea wataalamu kutoka IITA katika kata ya Mwika Kusini, Wilaya ya Moshi Vijijini
Achibold Masimba mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea
jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya
Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia
mradi wa N2AFRICA
Elizabeth Paschal mkulima wa maharagwe Kijiji cha Kireweni Kata ya Mwika Kusini akielezea
jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya
Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia
mradi wa N2AFRICA
Mtaalamu wa kilimo kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika kusini Elizabeth Josiah akielezea jinsi wakulima wanavyonufaika na kilimo cha maharagwe
Ester Mbando (kulia) Mkulima wa maharagwe Kijiji cha Mawanjeni Kata ya Mwika Kusini akielezea
jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya
Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia
mradi wa N2AFRICA
Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa.
Mkulima wa zao la maharagwe Joseph Towo kutoka Kijiji cha Rauya Kata ya Marangu Mashariki akielezea
jinsi alivyonufaika na mbegu za maharagwe zilizotolewa na Taasisi ya
Kimataifa ya Utafiti wa mazao ya kilimo cha Kitropiki (IITA) kupitia
mradi wa N2AFRICA
Wanufaika wa mradi wa N2AFRICA wakielezea namna walivyonufaika na kilimo cha maharagwe
Fredy Urio akisimulia changamoto alizokabiliana nazo kabla ya mradi huwa kuwasili kijijini kwao na kuwa na manufaa kwa wakulima
Afisa kilimo Kata ya Mwika kusini Wilfred Ngileakielezea jinsi wakulima walivyonufaika na Mradi wa N2AFRICA katika kata hiyo
Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa.
Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akielezea jinsi alivyonufaika na kilimo cha maharagwe na hatimaye kununua mbuzi saba wa maziwa. Wengine ni wataalamu kutoka IITA na Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal
Mkulima wa zao la maharagwe Kamili Minja akionyesha shamba lake jinsi lilivyostawi kutokana na mafunzo ya kilimo bora kwa kutumia mbegu bora za maharagwe
EmoticonEmoticon