Mkuu wa Kitengo cha Huduma bora za benki ya UBA, Ms Queen Odunga (Kushoto) akizungumzia namna ya Kituo cha huduma kwa Wateja kitakachokuwa kikifanya kazi kwa masaa 24 kila siku katika kuhakikisha kuwa UBA Tanzania inaendelea kutoa huduma bora na zenye kuendana na matakwa ya wateja wa UBA Tanzania. Uzinduzi huo umefanyika Mapema leo katika ofisi za makao makuu ya benki hio zilizopo barabara ya Mwl Nyerere, Jijini Dar Es Salaam.Pembeni ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Peter Makau.
Mkuu wa idara ya Uendeshaji wa Benki ya UBA Tanzania, Bw Chriss Byaruhanga akizungumzia juu ya Uzinduzi wa Kituo Kipya cha Huduma kwa Wateja cha Benki ya UBA Tanzania Kitakachokuwa kikifanya kazi kwa Masaa 24 kila siku.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya UBA Tanzania, Mr Peter Makau akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)mapema leo wakati wa kuzindua kituo cha huduma kwa wateja cha benki ya UBA Tanzania kitakachofanya kazi kwa masaa 24 kila siku.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki ya UBA Tanzania, Bi Brendansia Kileo akifafanua Juu ya huduma nyingine zinatolewa na benki hiyo huku lengo kubwa likiwa ni kuwafikia wateja wengi zaidi na kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wao.
Dar Es Salaam, Benki ya UBA Tanzania leo (Jumatano) imezindua kituo cha Huduma Kwa Wateja Cha Masaa 24 Kila Siku. Kituo hiko kitakuwa kikifanya kazi kwa masaa 24 kila siku huku lengo likiwa ni kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wao na wasio wateja muda wote pale ambapo mteja anahitaji huduma kutoka benki hio.
Kituo hiko cha Huduma kwa Wateja kwa Masaa 24 kitakuwa kikitoa huduma pia kupitia mitandao yao ya Kijamii ya Facebook, Twitter, BBM, E-mail na kupitia simu ya meza.
Ili mteja aweze kupatiwa huduma anapaswa kuwasiliana nao kwa njia mojawapo kati ya hizi kwa kutumia barua pepe (e-mail: CFC@ubagroup.com, Kupitia mtandao wa twitter Mteja anaweza kuwasiliana nao kupitia https://www.twitter.com/ubacares na kupitia facebook unaweza kuwasiliana nao kwa kutembelea https://www.facebook,com/ubaTanzania na instagram https://www.instagram.com/ubacares
Vilevile mteja anaweza kuwasiliana nao moja kwa moja kupitia namba ya simu ya +255 764 700 782 na kwa wale wanaotumia BBM basi wanapatikana kupitia BBM channel C00211246
Pamoja na kuzindua kituo hiko cha huduma kwa wateja kwa masaa 24 siku 7 za wiki vilevile UBA Tanzania wanatarajia kufungua matawi mapya manne ili kupanua wigo na kuwafikia wateja wengi zaidi na kuwasogezea huduma karibu.
EmoticonEmoticon