SPIKA
Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF), Anne Makinda, amewataka watanzania kutumia Mfuko wa Taifa
wa Bima hiyo ili kupata unafuu wa matibabu pindi wanapougua.
Wito
huo alitoa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti huyo wakati alipozindua
kitengo cha kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika
Hospitali ya Kairuki.Alisema,
kutokana na gharama ya matibabu kupanda kila siku,kadi za bima ya afya
zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupata unafuu wa matibabu kipindi mgonjwa
anapokuwa hana fedha.
Makinda,
alisema bima hiyo inatoa fursa kwa wanachama kupata huduma za matibabu
katika hospitali wanazoona zinatoa huduma nzuri na kumjali mgonjwa.
“Vituo
vyenye huduma ya NHIF vinapaswa kutibia wagonjwa kwa kuwajali ,
kuwapenda pamoja na kuwa wakarimu kwa wagonjwa kwani huduma hii
inasaidia sana watu hasa wale wanaougua magonjwa yenye kulipia gharama
kubwa,”alisema Makinda.
Aidha
alisema ni watu wachache ambao wanauwezo wa kujitibu bila bima ya afya
lakini watu wengi wanategemea huduma hiyo kulingana na gharama kubwa za
matibabu katika baadhi ya magonjwa.
Kwa
Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kairuki Dk. Asser Mchomvu,
alisema nchini Tanzania watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa
yanayosababishwa na matatizo ya figo.
“Kwa
hivi sasa ugonjwa huo umeonekana kuathiri kati ya asilimia 7 hadi 13
ya watanzania, wengi wao wakiwa wagonjwa wa kisukari (Diabetes
Mellitus)na shinikizo la damu(Acute Kidney injury) ,”alisema.
Alisema
kwa muda mrefu hospitali yao imekuwa ikipokea wagonjwa wenye matatizo
ya figo na kulazimika kuwapa rufaa kwenda nje ya hospitali hivyo kupitia
kitengo hicho kitaweza kutibu wagonjwa 40 kwa siku.
Alisema
kuwa kutakuwa na mashine 10 zenye uwezo wa kuwahudumia wagonjwa na
hadi kufikia sasa wamepata kibali cha wizara husika ambapo miongoni mwa
mashine hizo ipo ya kuchuja damu itakayosaidia kuzuia uharibifu wa figo
wa kudumu na wa muda hivyo kuokoa gharama.
Dk.
Mchomvu, alisema hospitali hiyo inatarajia kuongeza idadi ya mashine
ili kuweza kuwahudumia wagonjwa wengi pamoja na kutoa huduma ya
kupandikiza figo na kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHJF), Anne Makinda
(katikati), akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali,
Kokushubila Kairuki (kushoto), wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja
Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Kairuki Hospitali.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kairuki Hospitali Dk. Asser Mchomvu, akitoa hotuba yake wakati
wa uzinduzi wa Kitengo cha kuchuja Damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya
figo cha Kairuki Hospitali.
Baadhi ya madaktari waliohudhuria hafla hiyo wakisikiliza hotuba za viongozi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki Hospitali, Kokushubila Kairuki akitoa hotuba yake.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda
(kushoto), akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Kitengo cha Kuchuja Damu
kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo cha Hospitali ya Kairuki Mikocheni
jijjini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kairuki,
Kokushubila Kairuki.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda
(kushoto), akipata maelezo alipotembelea kitengo cha kuchuja damu kwa
wagonjwa wenye matatizo ya figo.
Dk. Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda.
Dk. Muga akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda
(katikati), akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi wa Kitengo cha Kuchuja
Damu, Eva Beatus.
Jengo la Kitengo hicho.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne Makinda, akitoa hotuba yake.
EmoticonEmoticon