Meneja
na mtaalamu wa masuala ya kemikali kutoka Taasisi ya Envirocare,
Euphrasia Shayo (kulia) akiwasilisha mada yake juu ya madhara ya
kemikali za vipodozi na mkorogo kwenye Tamasha la Jinsia Tanzania 2017
Mmoja wa washiriki katika warsha hiyo akiuliza swali mara baada ya uwasilishaji.
Afisa Utafiti na Uchambuzi wa TGNP, Maureen Mbolene akitoa maelekezo kwa washiriki wa washa hiyo.
Sehemu ya washiriki katika semina hiyo.
Sehemu ya wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya jamii wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 wakifuatilia mada anuai toka kwa wawasilishaji. |
MATUMIZI ya
vipodozi vyenye kemikali ya sumu yamewatisha wakulima katika Tamasha la
Jinsia Tanzania 2017 linalofanyika katika viwanja vya TGNP Mtandao,
Mabibo jijini Dar es Salaam.
Hofu
hiyo ilitanda jana baada ya Meneja na mtaalamu wa masuala ya kemikali
kutoka Taasisi ya Envirocare, Euphrasia Shayo kuwasilisha mada yake kwa
kundi hilo la wakulima wanaoshiriki tamasha la jinsia kutoka maeneo
anuai.
Alisema
kemikali za sumu kama zebaki na mericuri zilizomo katika vipodozi na
mikorogo isiyo rasmi inayotumiwa hasa na akinamama kujichubua na
kubadili nyele zao zina madhara makubwa katika kilimo.
Alisema
kemikali hizo mbali na kukaa ardhini kwa muda mrefu zaidi zikiharibu
mazao pia vinamadhara makubwa kwenye miili yao, hivyo kuwashauri
kuachana navyo mara moja kwa watumiaji.
Alisema
kemikali hizo mara baada ya kutumiwa hutelekezwa ardhini na mara mvua
zinyeshapo husafirishwa hadi katika vyanzo mbalimbali vya maji hivyo
kujikuta vikitumiwa tena na jamii jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya
binadamu na mifugo.
“…Vinamadhara
makubwa katika miili yetu, ndio maana sasa hivi magonjwa ya ajabu ajabu
ikiwemo kansa vimeendelea kushamiri kwetu, vinginea husababishwa na
kemikali hizi zenye sumu. Wapo akinamama wameathiriwa vibaya sana na
kemikali hizi zenye sumu,” alisema Bi. Euphrasia Shayo.
Kwa
upande wao baadhi ya wakulima wakishiriki katika mjadala waliiomba
Serikali kuwatumia wataalamu kama Bi. Euphrasia Shayo kutoa elimu ya
madhara kwenye redio na luninga ili kila mmoja aelewe madhara ya
vipodozi hivyo.
Haya
hivyo waliiomba kuendeleza oparesheni la kuwakamata na kuwachukulia
hatua kali waingizaji wa vipodozi vyenye viambata vya sumu ili kupunguza
madhara kwa jamii.
EmoticonEmoticon