Afisa Utafiti na Uchambuzi wa TGNP, Maureen Mbolene akitoa maelekezo kwa washiriki wa washa hiyo.
Sehemu ya wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati
ngazi ya jamii wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017
wakifuatilia mada anuai toka kwa wawasilishaji.
Mwakilishi wa Forum CC, Jackson Massawe (aliye simama) akiwasilisha mada
kwa wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya jamii
wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017.
SERIKALI imeobwa kutoa kipaumbele katika upatikanaji wa
mikopo nafuu ya kilimo kwa wanawake, ikiwa ni pamoja na kupewa haki ya
kupata na kumiliki mashamba ili kuongeza tija katika uzalishaji wa
bidhaa za kilimo.
Kauli hiyo imetolewa na
Mwakilishi wa Forum CC, Jackson Massawe alipokuwa akiwasilisha mada kwa
baadhi ya wakulima, wachimbaji wadogowadogo na wanaharakati ngazi ya
jamii wanaoshiriki katika Tamasha la Jinsia Tanzania 2017 linaloendelea
katika viwanja vya TGNP Mabibo Dar es Salaam.
Alisema
Sekta ya Kilimo nchini Tanzania imebebwa na wanawake, na wao ni uti wa
mgongo katika nguvukazi ya kilimo Tanzania. Aliongeza kuwa wanawake
wanaoshiriki katika sekta ya kilimo ni takribani asilimia 70 kiwango
ambacho ni kikubwa ukilinganisha na wanaume.
Bw.
Massawe aliishauri Serikali kuongeza bajeti katika sekta ya kilimo huku
ikiwa na mrengo wa kijinsia, huku ugawaji wa fedha za bajeti ufanyike
kama ilivyokusudiwa.
Naye, Mwakilishi kutoka
Taasisi ya Ekama, Lucia Akaro akiwasilisha mada ya Ukatili wa jinsia
kwenye kilimo alisema bado idadi kubwa ya wanawake wamekuwa wakikabiliwa
na vitendo hivyo katika gazi za familia.
Alisema
kuna kila sababu vitengo husika kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari za
ukatili wa jinsia, hasa kwa kundi la wanaume katika mapambano ya
kuhakikisha ukatili wa jinsia unapingwa vikali na makundi yote.
"...Wanawake
wengi hukumbana na ukatili wa jinsia ambao unasababishwa mara nyingi na
wanaume kuanzia ngazi ya familia ikiwa ni pamoja na kumnyima mwanamke
uhuru wa kufanya maamuzi katika ngazi ya familia hususani kwenye kipato
cha familia. Hii husababishwa na miiko na majukumu ya kijinsia na
kutokuwa na nguvu sawa kati ya mwanaume na mwanamke.,"
Aidha
alizitaja changamoto zingine zinazowakabili wakulima ni pamoja na mvua
zisizo za uhakika, kupotea kwa vyanzo vya maji na mlipuko wa magonjwa
kwa mimea na mifugo kama vile kanitangaze na mnyauko.
Aliitaka
Serikali pia kukabiliana na changamoto zinazotokana na mabadiliko ya
tabia nchi, kundi la wanawake ndilo linaloathika zaidi na mabadiliko ya
Tabianchi.
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mobile:- 0717
030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
EmoticonEmoticon