Muda wa Maongezi, SMS na Data za Bure kwa Wanunuzi wa Tiketi za ‘Tigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa’

September 05, 2017

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko Tigo, William Mpinga(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jana wakati wa kutangaza ofa maalum za vifurushi zitazotolewa ununuapo tiketi ya tamasha la Tigo Fiesta kwa njia ya Tigo pesa. Pembeni ni Afisa Biashara wa Tigo, Edwin Mgoa

Tigo inatoa dakika 100 za muda wa maongezi, SMS  100 SMS na and 100 Mbs za data kwa manunuzi yote ya tiketi kupitia TigoPesa



Dar es Salaam, Jumatatu 4 Septemba, 2017- Huku ikiwa imebakia siku chache tu kabla ya onesho la kwanza la msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa kufanyika jijini Arusha, wadhamini wakuu kampuni ya Tigo inazidi kutoa ofa kabambe kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za awali kupitia huduma ya TigoPesa.

Tigo inatoa dakika 100 za bure, SMS 100 za bure, na  kifurushi cha 100Mbs cha data bure kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zaoTigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa kupitia huduma ya TigoPesa.

Akitangaza ofa hiyo murwa jijini Dar es Salaam jana, Mkuu Mtendaji wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga alisema kuwa ofa hii mpya ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100Mbs za  data inaenda sambamba na ofa iliyopo sasa ya punguzo ya bei asilimia 10% kwa tiketi zote za awali za Tigo Fiesta 2017 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa au huduma ya kuhamisha fedha ya mitandao mingine yote ya simu nchini.

‘Kama tulivyoahidi hapo awali, tuna furaha kuthibitisha kuwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za ‘Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa’ kupitia Tigo Pesa, moja kwa moja watapata bonasi ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100 Mbs za data bure kutoka Tigo. Hii ni pamoja na ofa nono ya punguzo la 10% wanayopata wateja wote wa simu za mkononi wanaonunua tiketi zao za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya huduma ya kuhamisha fedha kwa njia ya mtandao wa simu.’

Aliongeza kuwa ofa hii inaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa na kuwajali zaidi wateja wake nchini.

Ili kununua tiketi za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya mtandao na kupata ofa hizi kabambe, mteja anahitaji kufuata hatua za kawaida za kutuma fedha na kutuma TZS 9,000/- kwenda namba 0678 888 888. Hapo mnunuzi atapokea ujumbe mfupi wa maneno (SMS) utakathibitisha kuhusu manunuzi yake ya tiketi pamoja na ofa za dakika 100 muda wa maongezi, SMS 100 na 100Mbs za data kutoka Tigo.
‘Napenda kuwaambia wateja wa Tigo wakae mkao wa kufaidika katika msimu huu wa Tigo Fiesta 2017 kwa sababu kuna ofa nyingi za kusisimua ambazo tutazitanganza katika siku zijazo,’ Mpinga alisema.


Mwaka huu msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa utajumuisha mikoa ya Arusha Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora na Dodoma. Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa pia itatua katika mikoa ya Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Moshi na Mtwara, kabla ya kuhitimishwa jijini Dar es Salaam.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »