Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiongea wakati wa kutambulisha shindano la mama msosi linalolaratibiwa na kituo cha radio Nuru FM 93.5 Iringa katika viwanja vya Kata ya Kihesa.
Msimamizi wa vipindi vya Nuru fm radio na ndio Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya mama msosi mkoani Gerald Malekela akiongea na hadhara iliyokuwa imejitokeza wakati wa utambulisho wa shindano hili
Baadhi ya washiriki wa shindano la mama msosi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati
Na fredy Mgunda, Iringa.
Shindano la mama msosi
linaloratibiwa na kituo cha radio cha Nuru fm mkoani Iringa limetambulishwa
rasmi kwa wakazi wa manispaa ya Iringa likiwa na lengo la kutoa elimu ya
utunzaji wa mazingira kwa kina mama na jamii kwa ujumla,shindano hilo litawapa
washindi kumi na nane kwa kila kata ya manispa ya Iringa ambapo kila mshindi
atajinyakulia mtungi mmoja wa shirika la gesi la mihan.
Akizungumza wakati wa
utambulisho wa shindano hilo mwenyekiti wa kamati ambaye pia ni msimamizi wa
vipindi vya Nuru fm radio Gerald Malekela alisema kuwa wameamua kutoa elimu ya mazingira kwa kuifikia jamii moja kwa moja
kwa njia ya kuandaa shindano ambalo limeanza kwa mafanikio makubwa.
“Kutoa elimu kuna njia nyingi sana hivyo nuru fm
radio 93.5 Iringa tumeamua kutoa elimu ya utunzaji wa mazingiri kwa wakazi wa
mkoa wa iringa kwa kutumia mashindano ya kupika na ndio maana unaona wananchi
wamejitokeza kwa wingi sasa nauhakika elimu ya utunzaji wa mazingira imewafika
na itaendelea kuwafikia” alisema Malekela.
Malekela aliwataka
wakinamama ambao hawajachukua fomu za kushiriki shindano hili walizuate kwenye
kata na hapa radio nuru fm ili kupata elimu bure ya mazingira ,ujasiliamali na
kujua jinsi ya kutumia nishati mbadala ambayo haina madhara makubwa kwa jamii
tofauti na ukataji miti hovyo.
“Mmekuwa mashaidi jinsi gani
akinamama walivyokuwa wanapata tabu kuwasha moto hapa kwa kuwa walikuwa
wanatumia mkaa,mmewaona walivyochafuka hivyo kama wangekuwa wanatumia gesi
hawagepata shida yote hiyo wala wasingechukua muda wote huo kupika” alisema
Malekela
Aidha Malekela alitaja
maeneo ambayo shindano la mama msosi litafanyikia ambazo ni kata zote kumi na
nane za manispaa ya Iringa hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza katika maeneo
ambayo shindano litakuwa linafanikia.
Akihudhuria utambulisho wa
shindano mama msosi linaloendeshwa na kituo cha radio Nuru fm mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati
aliipongeza radio hiyo kwa hatua waliyochukua kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira
kwa njia ya mashindano ambayo yameanza kwa kuwa na mashabiki wengi.
“Leo ni utambulisho tu lakini watu ni wengi na hamasa imekuwa kubwa
hivyo naamini kuwa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wakazi wa manispaa ya Iringa
itawafikia vilivyo na kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira ambao umekuwa
ukiathili mazingira kwa ujumla” alisema
kabati
Kabati aliongeza kuwa
ataendelea kuliunga mkono shindano hilo kwa kuwa linatija ya kimaendeleo kwa
taifa la Tanzania narudia tena kuwapongeza Nuru fm kwa wazo lenu ambalo
litaungwa mkono na watu wengine wadau wa mazingira.
Kwa upande wake meneja wa
kituo cha radio Nuru fm Victor Chakudika alimshukuru mbunge huyo kwa kuthamini
kitu kinachofanywa na rado kwa maendeleo ya wakazi wa mkoa wa Iringa na mikoa
yote inayoizunguka mkoa wa Iringa na kuwaomba wananchi kuendelea kusikiliza
radio Nuru fm kwa habari za uhakika,matukio mbalimbali na kwa burudani nzuri.
“Radio yetu inavijana wengi
wenye kuhitaji mafanikio na kuisadia jamii na ndio maana wamekuwa wakibuni vitu
mbalimbali vinavyoleta tija kwa maendeleo ya taifa hata ukikumbuka hivi karibu
tuliendelesha mashindano ya mpira wa miguu yaliyokuwa yanaitwa Ritta kabati
challenge cup na yalikuwa na mafanikio makubwa hivyo narudia tena kumshukuru
mbunge huyu” alisema chakudika
EmoticonEmoticon