Katibu
wa TASWA-ARUSHA Mussa Juma wa nne kutoka kulia akiwa pamaoja na
wadhamini wa muda mrefu wa bonanza la wanahabari mkoani Arusha mara
baada ya kumaliza mkutano na wanahabari ambapo wametangaza kuwa bonanza
la mwaka huu litafanyika siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa
Mwalimu Julius K. Nyerere
Waandishi wa Habari kutoka chuo cha uandishi wa Habari Arusha wakifurahia ushindi wao katika moja ya mabonanza yaliyopita jijini Arusha ambapo chuo hicho kimekuwa kikishriki bonanza hili toka mwaka 2008 na mwaka huu wamethibitisha kushiriki tena |
Baadhi ya Waandishi wa habari za michezo wakifatilia burudani katika moja ya bonanza la wanahabari za michezo jijini Arusha. |
Wakufunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha wakifuatilia mwenendo wa Mchezo kati ya Sunrise Redio na Chuo cha AJTC |
Mwandishi wetu,Arusha
Wanahabari
zaidi ya 400 wanatarajia kushiriki katika Tamasha la vyombo vya
habari, Kanda ya kaskazini, litakalofanyika kuanzia Octobar 14 siku ya
kumbukumbu ya mwalimu Julius Nyerere hadi octobar 15 mwaka huu.
Siku
ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere kutakuwa na kongamano kujadili
mchango wa hayati baba wa Taifa, katika masuala ya kiuchumi, kisiasa na
michezo na baadaye octobar 15 kutakuwa na michezo katika uwanja wa
General Tyre katika jiji la Arusha.
Tamasha
hilo ambalo hufanyika kila mwaka linaandaliwa na Taasisi ya Arusha
Media kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za michezo na
burudani mkoa Arusha(TASWA- Arusha chapter).
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Katibu wa TASWA mkoa Arusha, Mussa Juma,
alisema tamasha hilo litashirikisha wanahabari 400 kutoka mikoa ya Arusha,Manyara,
Kilimanjaro na Jijini Dar es Salam.
Juma
alisema katika kongamano hilo mada mbali mbali zitatolewa na wabobezi katika
masuala ya kiuchumi, kisiasa na michezo na wanahabari watapata fursa
kutambua zaidi mchango wa hayati baba wa Taifa katika michezo.
"Mwaka
huu, tumeamua kuanza na kongamano ili kukumbushana wanahabari masuala
mbali mbali ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu"alisema
Akizungumzia
maandalizi ya Bonanza, mratibu wa bonanza hilo Andrea Ngobole amesema katika tamasha hilo
wanahabari na timu waalikwa watashiriki katika michezo ya soka, kuvuta kamba,
mbio za magunia, riadha, kukimbiza kuku .
"maandalizi
yanakwenda vizuri lakini tunaomba wadhamini zaidi kujitokeza ili
kufanikisha tamasha na Kongamano la wanahabari mwaka huu"alisema.
Alisema
katika michezo timu ambazo tayari zimethibitisha kushiriki ni TASWA Dar
es Salaam ambao ndio mabingwa watetezi, timu za Radio Sunrise,timu za
vyuo vya Uandishi habari Arusha, Arusha one Radio, Triple A Radio, Radio
5, ORS Radio ya mkoa Manyara na TASWA Arusha.
"tutangaza zawadi hivi karibuni na pia wageni waalikwa kama ambavyo hufanyika kila mwaka"alisema.
EmoticonEmoticon