Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi
wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe (hawapo
pichani) leo alipofanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kupokea
maoni, ushauri na kusikiliza kero za watumishi wa umma Jijini Dar es
Salaam.
Mhudumu
wa Afya kutoka Hospitali ya Magomeni Bi. Rukia Mkapa akitoa malalamiko
yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati
wa kikao kazi na watumishi wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar
es Salaam.
Mwalimu
Paschal Mugayana kutoka shule ya Sekondari ya Njechele akitoa
malalamiko yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa umma wa Kata ya Kawe
kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya
Kawe wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati
wa kikao kazi na watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Ofisi
ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inaendelea
kusanifu na kuboresha Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara
(HCIMS) ili uweze kutumika kutoa taarifa za msingi kwa watumishi wa
umma wengi zaidi kwa lengo la kuleta mabadiliko ya utendaji kazi katika
sekta ya umma nchini.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi
na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni – Kata ya
Kawe, jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Kairuki amesema Mfumo wa HCIMS awali ulikuwa unapatikana Ofisi ya
Rais–Utumishi pekee, lakini baadae ukakasimishwa kwa Maafisa Utumishi
lakini sasa lengo ni kuwafikia watumishi wa umma waweze kuona taarifa
zao ili kupata taarifa sahihi na za uhakika katika kanzidata. Amesema
Tovuti ya Watumishi, Watumishi Portal, imeanzishwa maalum ili watumishi
wa umma wajisajili kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais-Utumishi yenye anuani
www.utumishi.go.tz na kuona taarifa zao za msingi.
Waziri
Kairuki, pamoja na hilo, amesema mfumo wa HCIMS umegatuliwa katika
Mamlaka za Serikali za Mitaa hivi sasa ili kurahisisha upatikanaji wa
taarifa na kufanya maamuzi kwa haraka zaidi.
“Kwa
kuwa mahitaji ya watumishi wa umma ni mengi hivyo tumeona ni vema
tukakasimu Mfumo huu na kwa watumishi wa umma katika kada nyingine ili
kurahisisha utendaji kazi na kuleta mabadiliko” Mhe. Kairuki amesema.
Waziri
Kairuki ameongeza kuwa tayari mafunzo kuhusu namna ya kutumia mfumo
yalikwishatolewa kwa Maafisa Elimu na Makatibu wa Afya wapatao 633.
“Tumeamua
kuanza na sekta hizi kwa sababu ni sekta zenye watumishi wa umma wengi
zaidi ukilinganisha na sekta nyingine lakini tutaendelea kugatua mfumo
wa HCIMS ili ufike katika sehemu nyingi zaidi za kutolea huduma (Service
Delivery Points).” Mhe. Kairuki ameongeza.
Mhe,
Kairuki yuko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es Salaam,
ambapo leo ni siku yake ya tano aliyoitumia kukutana na Watendaji na
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe.
Lengo
la ziara ni kukutana na watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko,
ushauri na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili
kuweza kuzifanyia kazi na kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma
nchini.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS-UTUMISHI
14.07.2017
EmoticonEmoticon