KAMPUNI ya Jamii Media ya Tanzania
wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na
Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la kuwakutanisha
wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania ikiwa
ni kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na mawasiliano
pamoja na kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja
wanaotumia huduma hizo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi
Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa
na matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo
likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa watumiaji. Alisema
wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa
sheria za kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa
kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa
watumiaji wa huduma za ICT.
Alisema wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria ya
Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila ya
uwepo wa kanuni jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na
wasimamizi wa sheria husika. Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media
itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za
mawasiliano wakiwemo bloggers ili kuona wanakuwa na uelewa na matumizi
mazuri ya mitandao yao kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika.
Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji kutoka 'Compass Communications Ltd' akiongoza majadiliano kwenye kongamano hilo.
Mmoja
wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza
kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo.
Kushoto ni Robert Madziva- Maxcom Africa wakifuatilia mjadala huo.
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
EmoticonEmoticon