Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John lipesi Kayombo akizungumza na wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakati wa ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Wananchi
pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifatilia kwa makini mkutano
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John lipesi Kayombo
akitafakari kwa makini changamoto mbalimbali za wananchi pamoja na wafanyabiashara katika soko la
Ndizi-Mabibo wakati wa ziara ya kikazi katika eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Kushoto) akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa ziara
ya kikazi katika soko la Ndizi-Mabibo
Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Ubungo wakifatilia mkutano wa Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika katika Soko la
Ndizi-Mabibo Jijini Dra es salaam
Wananchi
pamoja na wafanyabiashara katika soko la Ndizi-Mabibo wakifurahi mara baada ya kuambiwa wataendelea na shughuli zao katika soko hilo.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Ubungo amebaini ubadhirifu wa kiasi kikubwa cha pesa zinazofikia shilingi
milioni tisini kila mwezi, unaofanywa na kikundi kinachojiita Majimoto
kinachodai kupewa jukumu la kukusanya mapato katika soko la matunda la Mabibo
kwa niaba ya mmiliki wa eneo hilo ambaye ni Kiwanda cha Nguo cha Urafiki.
Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa ubadhirifu
huo umebainika baada ya Halmashauri ya Manispaa kuchukua jukumu la kusimamia
kwa muda ukusanyaji mapato katika soko hilo ambapo makusanyo yamepanda kutoka
shilingi milioni saba zilizokuwa zinakusanywa hapo awali hadi zaidi ya shilingi
milioni mia moja.
Kayombo amesema hayo wakati wa ziara
ya ghafla iliyofanyika sokoni hapo na kuongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe
Kisare Makori kwa ushirikiano wa pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo sambamba
na watendaji wote katika Manispaa hiyo,
Ziara hiyo imejili mara baada ya
uongozi wa kiwanda cha Urafiki kutaka kuwaondoa kwa nguvu wafanyabiashara na
kulifunga eneo hilo kwa kujenga uzio utakaozuia ufanyaji wa biashara.
Mkurugenzi amejibu hapo hapo agizo
la Mkuu wa Wilaya Mhe Makori lilomtaka kusitisha mara moja zoezi la kuwaondoa
wafanyabiashara hao kwa kuwaagiza Afisa Afya na Mazingira wa Manispaa ya Ubungo
kufuatilia malalamiko yaliyotolewa na wananchi katika mkutano huo kuhusu kiwanda
cha nguo cha Urafiki ambacho kinalalamikiwa na wananchi kwa kuathiri afya zao
kutokana na Moshi unaotoka kiwandani hapo.
Aidha
mbele ya umati wa wafanyabiashara na wananchi katika mkutano huo Mkurugenzi
Kayombo amemuagiza Kaimu Injinia wa Manispaa ya Ubungo kusambaza kifusi cha
mawe kilichomwagwa sokono hapo kwa ajili ya kuzuia mlundikano wa maji.
Mkurugenzi
Kayombo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria
kukusanya mapato kwa kiasi kikubwa hivyo ameeleza dhamira yake ya kukusanya
mapato ya Zaidi ya shilingi milioni 150 kwa mwezi katika soko la Ndizi-Mabibo
na tayari mirija na mianya yote ya rushwa amefanikiwa kuiziba kwa kiasi
kikubwa.
EmoticonEmoticon