Meneja wa TBL kiwanda cha Arusha,Joseph Mwaikasu akimpatia maelezo
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Tizeba utekelezaji wa kushirkiana na wakulima unavyofanyika
.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Tizeba(kushoto)akimsikiliza Afisa Ugani kutoka TBL Group,Joel Msechu(kulia)
Wakulima wa Shahiri kanda ya kaskazini wakijifunza mbinu za kilimo bora katika maadhimisho ya siku yao15.Waziri wa Kilimo,Dk.Charles Tizeba akiongea na baadhi ya wakulima wilayani Monduli
Wakulima wa Shahiri kanda ya kaskazini wakijifunza mbinu za kilimo bora katika maadhimisho ya siku yao15.Waziri wa Kilimo,Dk.Charles Tizeba akiongea na baadhi ya wakulima wilayani Monduli
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Tizeba(kushoto)akimsikiliza akitoa maelezo kwa wakulima wa zao la shayiri
……………………………………………………………………………………………
-Wakulima wa shahiri waanika mafanikio waliyoyapata
Wakulima
wa zao la Shayiri kanda ya Kaskazini wanaoshirikiana na kampuni ya TBL
Group wameeleza kuwa ushirikiano huo umewawezesha kupiga hatua mbalimbali za maendeleo kwa kuwa wanafanya kilimo wakiwa na uhakika wa kuuza mazao yao kwa bei nzuri.
Akiongea
kwa niaba ya wakulima wenzake katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa
Shayiri kanda ya kaskazini yaliyofanyika katika Kijiji cha Emairete wilayani Monduli juzi,
Mwenyekiti
wa umoja wa wakulima hao ,Bariki Kivuyo,alisema kuwa wanawezeshwa
kuanzia kupatiwa mbegu,utaalamu wa kutunza mashamba na kupatiwa madawa
na pembejeo za kilimo.
“Uwekezaji
wa kampuni ya TBL Group katika kilimo ni mkakati ambao umesaidia
wakulima wengi ambao hivi sasa wanafanya kilimo cha Shahiri kwa njia za
kisasa na uzalishaji umeongezeka zaidi ambapo kwa sasa wanavuna gunia kumi hadi 16 kwa heka moja badala ya gunia tano walizokua wanapata na kwa kuwa soko ni la uhakika maisha
ya wakulima wengi yamebadilika kuwa bora kwa kujenga nyumba
nzuri,kusomesha watoto wao na kununua pembejeo za kisasa za
kilimo”.Alisema Kivuyo.
Hata hivyo alizitaja changomoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na miundombinu mibovu ya barabara inayoongeza gharama
za ziada kwa wakulima kusafirisha mazao kutoka shambani kwenda
kiwandani na kuiomba serikali iimarishe barabara zinazoingia na kutoka
kwenye mashamba makubwa.
“Tunaomba
mapato yanayolipwa kwa halmashauri sehemu yake irudishwe kwenye vijiji
vinavyolima Shayiri kwa wingi ili kuhamasisha zao hili ili kuchochea
kilimo kikubwa zaidi na kuwapunguzia wakulima mzigo na kufanikisha
mkakati wa serikali ya awamu ya tano wa kuwawezesha wananchi hususani wenye kipato cha chini,”alisema Kivuyo
Kwa
upande wake Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi,Dk Charles Tizeba,ambaye
alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ameitaka kampuni ya TBL Group kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya ambapo kuna kilimo cha Shayiri
kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji ili serikali isitishe kuagiza
kimea nje ya nchi na aliwataka maafisa kilimo kuweka mipango madhubuti
ya kilimo hicho ili kuwawezesha wakulima kunufaika zaidi.
Alipongeza juhudi za kampuni ya TBL
kuwawezesha wakulima pembejeo na utaalamu katika kilimo cha mikataba
kinachowahakikishia wakulima soko la mazao yao na kutaka halmashauri
kupitia vyama vya ushirika wa wakulima kuwawezesha wakulima kuingia
mikataba yenye tija kwao.
Awali
Meneja wa kiwanda cha TBL mkoa wa Arusha,Joseph Mwaikasu, alisema
jitihada za kuwawezesha wakulima kuongeza ubora na kiwango cha Shayiri
unaendelea kwani wamekua wakipata zao hilo chini ya kiwango cha mahitaji
yao.
Alisema
mahitaji ya kampuni kwa mwaka ni tani 18,000 lakini wakulima wanaweza
kuzalisha tani 10,000 pekee na zinazobaki wanaagiza nje ya nchi hivyo
kuwataka wakulima kuongeza uzalishaji kwa manufaa yao na taifa kwa
ujumla.
Alisema
katika kipindi cha mwaka 2016 TBL imewalipa wakulima katika mikoa hiyo
Sh 14.7 bilioni zilizotokana na tani 12,700 wakati mwaka huu
wameshawakopesha wakulima Sh 2.1 bilioni ziwawezeshe katika maandalizi
ya shamba pamoja na pembejeo.
Mwaikasu
alisema TBL Group kupitia mkakati wake wa ‘Dunia Maridhawa’ moja ya
malengo yake ni kujenga dunia inayokua hivyo itaendelea kufanya kazi na
wakulima kama
ambavyo hatua hii imeanza kuleta mafanikio kwa kuboresha maisha ya
wakulima,kupanua wigo wa ajira kutokana na mpango huu na kampuni
kunufaika wa kupata malighafi bora inayozalishwa hapa nchini.
EmoticonEmoticon