SERIKALI WILAYANI KOROGWE YAAPA KUKOMESHA MIMBA ZA UTOTONI

June 27, 2017
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi
Robert Gabriel akizungumza wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative kulia ni Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu na 
Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada
nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka
Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu kushoto akizungumza katika halfa hiyo kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka
Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka akizungumza katika halfa hiyo
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini,Gorge Nyaronga akizungumza katika halfa hiyo  
MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi
Robert Gabriel kushoto akimpatia zawadi ya kitenge

Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu akimshukuru kwa msaada wa ujenzi wa madarasa na vyoo na uzio
Founder wa A Better World Canada Eric Rajabu katikati akitazama kitenge chake
Risala ya shule hiyo ikisomwa

 Sehemu ya vyumba vya madarasa vilivyojengwa


 Wanafunzi wa shule ya Msingi Jitengeni  wilayani Korogwe wakitumbuiza wakati wa hafla hiyo
 MKUU wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kisherikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative


SERIKALI wilayani Korogwe Mkoani Tanga imepania kuhakikisha wanakomesha vitendo vya mimba za utotoni kwa kuwachukulia hatua kali watakaobinika kuhusika na matukio hayo ili kuweza kuondosha hali hiyo kwenye jamii.

Lakini pia imesema watakaohusika kuwa kichocheo cha ndoa hizo zifanyike wakiwemo wazazi kutoka pande zote mbili watafikishwa mahakamani ili sheria zichukue mkondo wake zaidi kwa lengo la kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe ,Mhandisi,Robert Gabriel wakati makabidhiano ya vyumba vya madarasa vitano na vyoo ishirini na nne,mradi maji na uzio wa shule ya msingi jitengeni iliyopo Mji mdogo wa Mombo uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali A better World ya Canada ikishirikiana na Vuga development Initiative
.

Alisema hatua hiyo ina lengo la kuhakikisha wanakomesha vitendo vinavyofanya na baadhi ya vijana vya kuwa sha wishi wananfunzi wa kike na kuwapatia ujauzito hivyo kupelekea wasichana hao kukatisha masomo yao.

Mkuu huyo wa wilaya alisema hivi sasa  lazima wawe wakali na watu wanaocheza na maisha ya watoto ya wanafunzi ambao asilimia kubwa masomo yao yana haribiwa mara tu baada ya kushawishiwa na kupewa ujauzito.

Alisema hatua ya kurubuniwa watoto wa kike kwenye masomo haiwezi kuvumiliwa hasa kipindi hiki ambacho hawatakuwa na nafasi tena ya kujiendeleza katika shule za serikali pindi watakapo jifungua.

Awali akizungumza wakati wa hafla hiyo ,Mkuu wa shuele ya msingi Jitengeni,Mafikiri Twinzi alisema umalizikaji wa madarasa hayo utapunguza kero kwa wanafunzi shuleni hapo ambapo awali walikuwa wakikaa wanafunzi 100 hadi 120 kwenye chumba kimoja.

Alisema shule hiyo iliyo na wanafunzi 816 imekuwa na tatizo la
uchakavu wa madarasa hali iliyopelekea kuwajengea woga wanafunzi wa kuangukiwa na kuta za shule hiyo.

Naye kwa upande wake,Mkurugenzi wa Taasisi ya A Better Worild Canada nchini Tanzania,Aizidi Kaoneka alisema taasisi hiyo lengo lake ni kuisadiana na  serikali katika kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu,afya na maji.

Aidha alisema baada ya kumalizika kwa ujenzi wa madarasa hayo,matundu ya vyoo,uzio pamoja na kuweka mabomba ya maji na sasa mpango uliopo ni kuendelea kuvunja madara manne mengine yaliyochakaa shuleni hapo ili kujenga upya na kutoa fursa kwa wanafunzi kujisomea bila kuwepo kwa vikwazo vya aina yeyote ile.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »