Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na watumishi wa iliyokuwa
Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata picha ya pamoja na na
watumishi wa iliyokuwa Presidential Delivery Bureau (PDB) waliokuwa
wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRNalipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na na watumishi wa iliyokuwa
Presidential Delivery Bureau (PDB)waliokuwa wakisimamia utekelezaji wa
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la wataalam wa masuala ya
umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha
umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa
uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na jopo la wataalam wa masuala ya
umeme na ujenzi wa miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha
umeme na kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa
uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 27, 2017
PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Juni, 2017 ameagana
na wafanyakazi wa iliyokuwa Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji wa Utekelezaji
wa Miradi (President’s Delivery Bureau – PDB) ambao wamehamishiwa katika ofisi na taasisi nyingine za Serikali kwa ajili ya kuendelea na utumishi wa umma.
Wafanyakazi hawa ndio walikuwa wakisimamia utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN).
Mhe. Rais Magufuli amekutana na
wafanyakazi hao Ikulu Jijini Dar es Salaam ambapo amewashukuru kwa kazi
nzuri waliyoifanya wakiwa PDB na amewataka kuendelea kulitumikia Taifa
kwa juhudi na maarifa wakiwa katika ofisi nyingine walizopangiwa.
“Natambua kuwa nyie ni
wafanyakazi wazuri wenye ujuzi na maarifa muhimu kwa ajili ya Taifa
letu. Mmetoa mchango mkubwa mlipokuwa PDB nategemea mtaendelea hivyo na
hata zaidi katika ofisi mbalimbali mlizopangiwa, mkachape kazi kwa
kutanguliza maslahi ya Watanzania” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mkutano huo umehudhuriwa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe.
Angellah Kairuki na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora Dkt. Laurian Ndumbaro.
Wakati huo huo, Mhe. Rais
Magufuli amekutana na timu ya wataalam wa masuala ya umeme na ujenzi wa
miundombinu ya mabwawa ya maji kwa ajili ya kuzalisha umeme na
kujadiliana nao kuhusu utekelezaji wa mradi mkubwa wa uzalishaji wa
umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge Power Project) ambao una uwezo wa kuzalisha Megawatts 2,100 za umeme.
Mhe. Rais Magufuli amekutana na
wataalamu hao ikiwa ni utekelezaji wa nia yake ya kuhakikisha mradi huo
unaanza kujengwa haraka iwezekanavyo na kuzalisha umeme mwingi
utakaosaidia kuharakisha maendeleo hapa nchini, hususani ujenzi wa
viwanda.
“Kesho Waziri Mkuu wa Ethiopia
Mhe. Hailemariam Desalegn anawatuma wataalamu wake waliojenga mradi
mkubwa wa bwawa la maji la kuzalisha umeme kule Ethiopia, wakiwa hapa
mtakutana nao na mtabadilishana uzoefu, nataka na sisi tusichelewe,
tuzalishe umeme utusaidie kwenye ujenzi wa viwanda” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
27 Juni, 2017
EmoticonEmoticon