UMMY MWALIMU AMPONGEZA NA KUMSHUKURU RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI

June 27, 2017
IGA1
Matukio mbaljmbali zikionyesha matukio wakati wa ugawaji Viuadudu vya  kutokomeza Mbu wa Malaria Mjini kibaha.Pichani ni Waziri Ummy Mwalimu akigawa Viuadudu hivyo kwa Halmashauri kumi na moja
IGA2Na. Catherine Sungura na Benson Mwaisaka,WAMJW- Kibaha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amempongeza na kumshukuru  Mhe.Dkt. John Pombe  Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa  kuongeza chachu katika mapambano dhidi ya malaria kwa kununua lita laki moja na kusambazwa kote  nchini.
Ameyasema hayo wakati wa ugawaji  wa Viuadudu vya kutokomeza mbu wa malaria kwa halmashauri kumi na moja zilizofika katika kiwanda cha kuzalisha Viuadudu hivyo kilichpo Mjini Kibaha

Aidha ,Waziri Ummy  alisema anamshukuru Mhe. Rais kwa kumruhusu kuanza zoezi hilo kwa awamu ambapo kwa awamu ya kwanza Viuadudu hivyo vitagawiwa kwa Halmashuri 14 nchini ambazo zina viwango vikubwa vya maambukizi ya ugonjwa wa malaria,“hii ametupa  nguvu na ari sisi tuliopo kwenye dhamana ya kusimamia sekta ya afya katika kupambana na Malaria.
Hata hivyo alisema kwa mujibu wa takwimu toka ofisi ya Takwimu nchini zinaonyesha kwamba kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa  Malaria nchini ni asilimia 14 ambapo katika kila watoto walio chini ya miaka mitano kati ya watoto 100 watoto 14 wamekutwa na maambukizi ya Malaria
“Maelekezo yangu hasa kwa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni kuhakikisha dawa hii mnapulizia kuzingatia  miongozo  iliyotolewa na  Wizara ya Afya,Muangalie ukubwa wa eneo la mazalia ya mbu,na kiasi kinachotakiwa kupulizia”.
Waziri Ummy amewataka wahakikishe wanapulizia Viuadudu hivyo angalau mara nne kwa mwezi kwa maana kila baada ya siku saba,hivyo ni lazima wanunue vifaa vya kupulizia dawa hii pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi watakaenda kufanya  zoezi hilo.
Pamoja na hayo Waziri Ummy aliwataka ifikapo mwisho wa mwezi huu kila Mkurugenzi wa Halmshauri awe ampelekee mahitaji halisi ili kuona ni jinsi gani watatekeleza kazi hiyo “Lazima nipate mahitaji halisi toka Halmashauri kwa kuwa Mhe. Rais ameshatuonyesha njia na ametuelekeza badala ya kununua dawa pia tununue na  viuadudu hivi”
Naye Mkurugenzi Msaidi toka Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi Elli Pallangyo alisema leo hii Halmashauri kumi na moja  sawa na Mikoa sita ndizo zilizofika katika uzinduzi huo wa ugawaji wa Viuaduddu kwa awamu ya kwanza,alizitaka Halmashauri hizo na mgawanyo wa lita kwenye mabano
Liwale(1,200), Tarime (384), Misungwi(1,296), Kasulu(540), Songea(816),Kakonko(660), Kisarawe(720), Kyerwa(1,080), Rufiji(5,088), Geita(2,100), Kilombero(1,140)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »