Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye
ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na
kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.
Akizungumza,
leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya
miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja
wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.
“Tunapoadhimisha
miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na
kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama
Pia,
Waziri Mhagama aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa
wingi katika Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa
wake umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia
alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya
maadhimisho hayo.
“Wananchi
wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano,
ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea
kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema
Rugimbana
Maandalizi
ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano yamehudhuriwa pia na Mkuu wa
Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme, pamoja na viongozi mbalimbali
wa Serikali.
Aidha,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia
yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na Serikali.
Maadhimisho
hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa namaonesho kutoka
kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama, burudani za vikundi vya
ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.
Waziri Mhagama akikagua maandalizi ya kuadhimisha Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri leo Mjini Dodoma.
Baadhi
ya wananchi wakifuatilia maonesho ya maandalizi ya Maadhimisho ya miaka
53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika
terehe 26 Aprili Mjini Dodoma kwa mara ya kwanza tangu Serikali
ilipohamia Dodoma.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya
maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya
maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya
maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Askari wa Pikikipi maalum wakionesha namna pikipiki hizo zitakavyopamba maonesho hayo.
Makomandoo
wa Jeshi la wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari
lenye tani 7 ikiwa ni moja ya mbinu ya medani katika uwanja wa
mapambano.
Askari wa Kikosi cha Farasi wakionesha umahiri wao katika kutumia farasi kupambana na uhalifu.
Wanafunzi wa halaiki wakipita kwa ukakamavu mbele ya Jukwaa Kuu.
EmoticonEmoticon