Dar Es Salaam – Usiku wa tarehe 20 Aprili katika Club ya Next Door ndani ya Masaki, Dar es Salaam, Castle Lite ilizindua promosheni ya 'Castle Lite Unlocks kwa mara ya kwanza Tanzania, na hivyo kuiweka nchi katika msisimko wa aina yake. Chumba kilikuwa kimejaa hamasa wakati Castle Lite ikimzindua Mfalme wa Muziki Kimataifa-FUTURE.
Uzinduzi huo ulishereheshwa na malkia mpya wa muziki wa pop na mtangazaji maarufu wa televisheni, Mini Mars, tangazo hilo lilibainisha kwamba Rapa ambaye ni mshindi wa tuzo ya “Turn On The Lights” atakuwa nyota katika onesho la Julai 22, 2017 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam, ambapo upatikanaji wa tiketi utatangazwa katika hatua nyingine zitakayofuata.
Castle Lite pia imetangaza kwamba mwanamuziki Diamond Platnumz atakuwa mshiriki mwenza katika tamasha hilo la Extra Cold Unlocks. Diamond Platnumz ni msanii wa kwanza Afrika Mashariki kusaini mkataba na kampuni ya kurekodi muziki ya Universal Music na hivyo kuwa mwanamuziki rasmi wa kimataifa.
“Ninawaahidi Watanzania burudani ya kipekee”, alisema Diamond Platinumz alipokuwa akizungumza kuhusu tamasha hilo.
Likiwa linawashirikisha wasanii wengine maarufu wa Kitanzania ambao watatangazwa katika hatua zitazofuata kuelekea katika tamasha hilo,
“Kampeni ya 'Castle Lite Unlocks' imekuwa kwenye harakati za maandalizi kwa miaka michache sasa, ambapo Castle Lite imebadili mfumo wa kawaida uliozoeleka kwa kuwaletea wasanii wa ngazi ya juu kimataifa ili kuburudisha nchini mbalimbali Afrika na kwa mara ya kwanza burudani inaletwa katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki jijini Dar es salaam alisema Mkurugenzi wa Masoko wa Afrika Mashariki, Thomas Kamphius.
"Tunaelewa kwamba wateja wetu sio kila mara wanapata fursa ya kuona baadhi ya matukio haya makubwa, hivyo tunataka kuwaletea fursa hii na kuendelea kuwaletea burudani za namna hii kwa miaka ijayo.Kamphius aliongeza.
Fuatilia matangazo mbalimbali katika vyombo mbalimbali vya habari , ikiwepo Radio, TV, mitandao ya kijamii na Magazeti ili kupata muendelezo wa matukio kutoka sasa hadi siku ya tamasha lenyewe Julai 22. Kwa hivi sasa chukua Castle Lite yako soma maelekezo jinsi ya kushiriki ili kupata fursa ya kushinda nafasi ya kuwa sehemu ya sehemu ya Burudani ya'Castle Lite Extra Cold Unlocks' ndani ya Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon