Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
(Kaunda suti nyeusi katikati)akipiga picha ya pamoja na Waheshimiwa
Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya
Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu na kamati
ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakiongozwa na Mhe. Douglas Syakalima,
ambae ni Mwenyekiti wa Kamati na Kiongozi wa Msafara/Ujumbe huo katika
kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
(wa pili kulia)akimkabidhi kitabu chenye Sheria Mbali mbali za Bunge
Mhe. Douglas Syakalima (wa pili kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa kamati
ya Miundombinu na Kiongozi wa Msafara wa kutoka Bunge hilo, Wabunge hao
wamekuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya
Miundombinu katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini
Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na kulia
ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mhe. Prof. Norman Sigala King.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni
Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja
kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika
kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge
la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Miundombinu kutoka Bunge
hilo wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati)akizungumza
katika kikao kilichofanyika leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma, Wabunge
hao walikuja kubadilishana uzoefu na kamati ya kudumu ya Bunge ya
Miundombinu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Miundombinu, Mhe. Prof. Norman Sigala King akizungumza na
Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Zambia ambao pia ni Wajumbe wa
kamati ya Miundombinu kutoka Bunge hilo waliokuja kubadilishana uzoefu
na kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, katika kikao kilichofanyika
leo Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)
EmoticonEmoticon