Waziri
wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (MB)
ameipongeza benki ya DCB kwa hatua kubwa waliyofikia ya kwa kuwa
miongoni mwa benki zilizoanzisha huduma zinazoendana na teknolojia ya
kisasa kama ilivyo kwa huduma za kibenki kwa njia ya mawakala (DCB
Jirani) na huduma za kibenki kwa njia ya simu za mkononi (DCB Pesa).
Simbachawene
amesema kufunguliwa kwa tawi hili zitasogeza huduma za kibenki karibu
na wafanyabishara na wakazi wa mji wa Dodoma na haya ndiyo maendeleo
tunayotaka katika sekta ya kibenki ili huduma za benki zipatikane kwa
urahisi zaidi kwa wananchi na nina hakika wananchi wengi watapata huduma
bora kupitia tawi hili.
Hivyo
nawaasa wafanyabiashara, wafanyakazi na wakazi wote wa mkoani Dodoma
watumie fursa hii kwa kufungua akaunti mbalimbali za DCB kupitia tawi
hili, ni imani yangu kwamba huduma zitakozotolewa na tawi hili zitakuwa
bora na zenye kumjali mteja.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa ametoa shukrani za
dhati kwa Mhe. George Simbachawene, Waziri wa TAMISEMI kwa kukubali kuwa
Mgeni rasmi katika hafla hii ikiwa ni mara yako ya pili kukubali wito
kuwa mgeni rasmi. Mara ya kwanza ilikuwa ni kuzindua rasmi tawi la
Benjamini Mkapa lililopo maeneo ya Samora karibu na ofisi za Halmshauri
ya Jiji la Dar es Salaam.
Mkwawa
amesema kwa upande wa Dodoma wamefanikiwa kupata mawakala 38 ambao
muda si mrefu wataanza kutoa huduma za DCB mitaa ya Dodoma karibu zaidi
na wananchi. Mbali na hapa Dodoma, pia wana mpango wa kupeleka huduma za
DCB mikoa mingine kupitia DCB Jirani kama vile mikoa ya Pwani,
Morogoro, Tanga, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kahama, Mtwara, Arusha,
Iringa na Mbeya lengo ni kuwa na mawakala 1,500 nchi nzima kufikia
Disemba mwaka huu.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka
ametoa wito kwa wakazi wote wa Dodoma na vitongoji jirani wazipokee
huduma za DCB na wawe mstari wa mbele kutumia huduma za benki tawini
hapo ili kukuza tawi hili na kuwa na uwezo mkubwa wa kuwahudumia
wananchi wengi zaidi katika suala zima la kupiga vita umasikini.
Prof
Msambichaka ameongezea na kusema wana imani wengi watanufaika na benki
hii kwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba mara kwa mara, kuimarisha
usalama wa fedha zenu na kujenga uwezo wa kupanua biashara kwa
kutegemea. Huduma hizi zina lengo la kusogeza huduma za kibenki karibu
zaidi na wananchi na kuongeza amana za benki ambazo ndio uti wa mgongo
wa benki zote duniani.
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene
(MB) akizundua tawi la Benki ya DCB mkoa wa Dodoma akishuhudiwa na
Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania John
Malecela(Kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa na
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka .
Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene
(MB) akizungumza kabla ya uzinduzi wa tawi jipya la Benki ya DCB mkoa
Dodoma na kuwapongeza kwa hatia kubwa waliyofikia ya kuendelea kutanua
huduma zao nje ya Mkoa wa Dar es salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa (kushoto) akisalimiana na Mgeni
rasmi Waziri wa Nchi ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. George Simbachawene
(MB) wakati akiwasili jengo la LAPF Mkoa wa Dodoma wakati wa uzinduzi wa
tawi la DCB mkoani humo. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Benki
ya DCB Prof . Lucian Msambichaka
Waziri
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania John Malecela
akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi la Benki ya DCB Mkoa wa Dodoma
na kuipongeza hatua kubwa waliyoifanya ya kutanua huduma mpaka mikoani
na kuwataka waendelee kufikiria na mikoa mingine. Ufunguzi huo
umefanyika leo Mkoa wa Dodoma.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya DCB Prof . Lucian Msambichaka
akizungumzia namna benki ya DCB ilivyoweza kujiendeleza kwa kipindi cha
miaka 15 na hatua kubwa waliyoifikia ya kufungua tawi Mkoa wa Dodoma.
Meneja
wa matawi ya Benki ya DCB mkoa wa Dar es salaam wakiwa wameenda
kushuhudia uzinduzi wa tawi la benki hiyo Mkoa wa Dodoma uliofanyika
leo.
Wafanyakazi wa Benki ya DCB mkoa wa Dodoma wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo leo Mkoani Dodoma.
Kikundi
cha Ngoma kutoka Mkoani Dodoma kikitumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa
tawi la Benki ya DCB Mkoa wa Dodoma uliofanyika leo.
Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Tawi la Benki ya DCB leo Mkoani Dodoma.
Waziri
Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania John Malecela akisaini
katika kitabu cha wageni wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya DCB leo
Mkoani Dodoma. Picha na Geofrey Adorph, Dodoma
EmoticonEmoticon