Droo ya pili ya biko

April 24, 2017
Msanii wa nyota wa filamu Tanzania, Kajala Masanja kulia, akichezesha droo ya pili ya kuwania Sh Milioni 10 ya mchezo wa Bahati Nasibu ya Biko 'Nguvu ya Buku' iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam ambapo mshindi wake Nicholaus Mlasu kutoka Ukonga Mombasa, Ilala alinyakua kitita hicho na kuhudhuriwa na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo mwenye kitabu mkoni. Katikati ni mshindi wa Biko wa wiki iliyopita, Christopher Mgaya. Picha na Mpiga Picha Wetu.

Nicholaus Mlasu azoa milioni 10 za Biko ‘Nguvu ya Buku’

Na Mandishi Wetu, Dar es Salaam
DROO ya pili ya wiki kutafutwa mshindi wa shindano la Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ ya kuwania Sh Milioni 10 imefanyika leo asubuhi huku mkazi wa Ukonga Mombasa, Ilala, jijini Dar es Salaam, ameibuka na ushindi huo na kuwa mtu wa pili kufaidika na mamilioni ya Biko, baada ya Christopher Mgaya kushinda wikiiliyopita na kukabidhiwa mamilioni yake.
Picha nyingine Kajala Masanja akimtangaza mshindi wa Biko wa wiki hii Nicholaus Mlasu kunyakua Sh Milioni 10 za Biko katika droo hiyo.

Mshindi huyo amepatikana katika droo iliyochezeshwa jana na Balozi wa Biko, Kajala Masanja pamoja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo pamoja na Mgaya mshindi wa wiki iliyopita.
Kajala Masanja na mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania kwenye notebook mkononi pamoja na mshindi wa wiki iliyopita, Chiristopher Mgaya wakiisoma namba ya mshindi wa wiki hii ambaye bwana Nicholaus Mlasu alitangazwa mshindi.

Akizungumza katika droo hiyo, Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, alisema kwamba ni furaha yao kubwa kuona wamempata mshindi mwingine aliyeshinda Sh Milioni 10 kutoka kwenye shindano lao linalofanyika kila mwisho wa wiki.

Alisema bahati nasibu ya Biko imezidi kujizolea umaarufu mkubwa kwa siku chache kutokana na urahisi wake wa kucheza pamoja na kutumia muda mdogo kulipa washindi wake, hususan wa zawazi za papo kwa papo zinazopatikana baada ya kucheza kwa kufanya miamala ya kifedha kwa simu za Vodacom, Tigo na Airtel Money.

“Ni rahisi kucheza Biko kwa sababu mtu anafanya muamala kwenye simu yake kuanzia Sh 1000 ambapo kwanza katika kipengele cha lipa bili, atakwenda kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 kisha ataweka 2456 kama namba yetu ya kumbukumbu.

“Baada ya kufanya hivyo mteja atapokea ujumbe wa maandishi katika simu yake kumjulisha hatua aliyofikia baada ya kucheza na tunashauri wateja wacheze biko mara nyingi ili wajiwekee nafasi nzuri ya kushinda kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Milioni 1,000,000 kama zawadi zetu za papo kwa hapo, pamoja kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ya wiki kuwania donge nono la Sh Milioni kumi (10,000,000) ambalo leo ndugu yetu Mlasu ameibuka na ushindi huo mnono,” Alisema Heaven na kumpongeza mshindi wao pamoja na kuwataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kuwania mamilioni ya Biko.

Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Jehud Ngolo alisema kwamba ni hatua nzuri kuona washindi wa Biko wanapatikana kila wiki sambamba na kupokea zawadi zao haraka.

“Bodi tunafarijika kwa sababu wale washindi wanapopatikana hupokea malipo yao kwa haraka hivyo wanaweza kuzitumia fedha zao katika mambo ya kimaendeleo na kujikwamua kiuchumi kwa kupitia mchezo wa Biko, hivyo nawaomba Watanzania waendelee kucheza biko ili wapate nafasi ya kuvuna fedha mbalimbali kwa kupitia bahati nasibu ya Biko,” alisema.

Naye mshindi wa Sh Milioni 10, Nicholaus Mlasu, alipokea simu ya ushindi kwa furaha na kusema amefurahishwa kwa sababu alikuwa akicheza Biko kwa malengo ya kushinda sambamba na kumuomba Mungu atimize maombi yake ili azoe mamilioni ya Biko.

Nimefurahi sana kwa kushinda Biko, namshukuru Mungu kwa kuniona maana sasa nimeweza kuibuka na mamilioni hayo ambayo nitayatumia vizuri maana ndio malengo yangu ya kucheza Biko kila siku ili niweze kushinda donge nono, alisema Mlasu.

Bahati nasibu ya Biko Ijue Nguvu ya Buku imezidi kushika kasi huku tayari ikiwa imeshamkabidhi mshindi wake wa kwanza Christopher Mgaya Sh Milioni 10 zake wiki iliyopita sambamba na kupewa elimu ya fedha kutoka benki ya NMB, Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »