Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Mfuko wa
Kukuza Sekta ya Fedha (FSDT) imewakutanisha pamoja wadau kutoka sekta
mbalimbali za maendeleo nchini kujadili masuala mbalimbali
yatakayosaidia uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo Tanzania.
Akizungumza
katika kikao kazi hicho mwenyekiti wa Kikundi Kazi, aliyewahi kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Peniel Lyimo alisema kuna haja ya
dhamira ya dhati na uwekezaji mkubwa katika sekta ya kilimo nchini ili
kusaidia juhudi za Serikali za kuinua ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini nchini.
Mwenyekiti
wa Kikundi Kazi, Bw. Peniel Lyimo (Katikati) akizungumza na wajumbe wa
Kikundi Kazi (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili
uwekezaji katika sekta ya kilimo uliofanyika katika Hoteli ya Court
Yard, Dar es Salaam. Wanaomsikiliza Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa TADB, Bw. Francis Assenga na Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa
FSDT, Bw. Mwombeki Baregu (Kulia).
Bw.
Lyimo alisema kuwa ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa
ajili ya maendeleo ya kilimo nchini unachangiwa kwa kiasi kikubwa na
mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa
biashara za bidhaa hali inayorudisha nyuma mapinduzi katika sekta ya
kilimo nchini.
“Kuna
haja ya kutafuta suluhisho la changamoto za upatikanaji wa fedha mikopo
kwa ajili ya Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha
kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na
kupunguza umaskini,” alisema.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akizungumza juu ya
umuhimu wa wadau katika kuchagiza uwekezaji katika sekta ya kilimo
nchini.
Akizungumzia
umuhimu wa kikao kazi hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw.
Francis Assenga alisema kikao hicho kinalenga kuwaleta wadau kutoka
sekta mbalimbali ili kujadili kwa kina njia sahihi za kuchagiza
uwekezaji wenye tija katika kilimo nchini.
Bw.
Assenga alisema kuwa kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo
kutachagiza kusaidia uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo, na kuleta
mapinduzi ya kilimo nchini.
“Kimsingi
Kikao hiki kinalenga kuanzisha mtandao mpana wa majadiliano na wadau
mbalimbali, zikiwemo Wizara zinazohusika na Kilimo na Taasisi mbali
mbali za Serikali na Binafsi, ili kukubaliana vipaumbele na namna ya
kushirikiana katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya TADB katika
kuleta mapinduzi ya kilimo nchini,” alisema.
Mkuu
wa Kilimo na Fedha Vijijini wa FSDT, Bw. Mwombeki Baregu (Kulia)
akizungumza wakati wa mkutano huo. Pichani ni Mwenyekiti wa Kikundi
Kazi, Bw. Peniel Lyimo (Katikati) na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Kilimo na Fedha Vijijini wa FSDT, Bw. Mwombeki
Baregu alisema kuwa FSDT inalenga kushirikiana na wadau ili kuchagiza
ushirikishaji mpana wa washirika mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi
ili kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini.
“Miongoni
mwa vikwazo katika kufikia ushirikishwaji wa fedha nchini Tanzania hasa
katika uwekezaji katika kilimo ni pamoja na ukosefu wa miundombinu
sahihi ya soko na upatikanaji wa fedha na huduma na bidhaa zake maalum
katika kilimo, hivyo tunaamini kwa kushirikiana na wadau tunaweza
kutatua changamoto hizi,” alisema Bw. Baregu.
Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa TADB, Bw. Albert Ngusaru akiwasilisha malengo ya mkutano huo.
Waumbe
wa Kikundi Kazi cha Kuchagiza Uwekezaji katika Sekta ya Kilimo nchini
wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.
Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini ya FSDT, Balozi Mwanaidi Maajar (Kulia) akitoa
mchango wakati wa Kikao Kazi cha Kuchagiza Uwekezaji katika Sekta ya
Kilimo nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Hazina na Utafutaji Fedha wa
TADB, Bw. Albert Ngusaru.
Mjumbe
wa Bodi ya Wadhamini ya FSDT, Balozi Mwanaidi Maajar (Kushoto)
akifurahia jambo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis
Assenga (Kulia) wakati wa Kikao Kazi cha Kuchagiza Uwekezaji katika
Sekta ya Kilimo nchini.
EmoticonEmoticon