Na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya
Kilimo,Mifugo na Uvivu imesema imeshughulikia malalamiko ya wakulima wa
Korosho kwa kuondoa makato yasiyokuwa muhimu katika zao hilo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara hiyo Mhe.William Ole Nasha wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.
“Serikali imekwisha fanyia
marekebisho maeneo ambayo wakulima walikuwa wanalalamikia kwa kuondoa
kabisa makato hayo katika zao hilo”, Aliongeza Mhe.Ole Nasha.
Amesema kuwa Serikali imefuta
ushuru wa shilingi 20 kwa kilo kwa ajili ya chama kikuu cha
Ushirika,Shilingi 50 za usafirishaji wa Korosho,Shilingi 10 kwa kilo
ajili ya mtunza ghala na pia shilingi 10 kwa kilo kwa ajili ya kikosi
kazi cha Masoko.Aidha Sekta ina utaratibu maalum wa kupanga bei dira kwa
kutumia vigezo vinavyokubaliwa kwa pamoja na wadau wote.
Kwa upande wa manunuzi ya pembejeo
za korosho amesema hufanywa kwa pamoja na vyombo rasmi ndani ya Tasnia
ambapo awali ilikuwa ikisimamiwa na mfuko wa Maendeleo ya Korosho na
sasa Bodi ya korosho Tanzania.
Aidha ameeleza changamoto
zinazojitokeza katika kufikisha pembejeo hizo kwa wakulima wa korosho na
hatua zimechukuliwa kwa kushirikisha vyama vya ushirika ili kudhibiti
mianya ya pembejeo kwenda kwa wasio lengwa.
Pia Serikali imeweka mfumo wa usambazaji wa pembejeo wenye lengo la kuhakikisha kwamba pembejeo hizo zinawafikia walengwa pekee.
“Utaratibu huu unazingatia
kutambua wakulima wenye uhitaji na pembejeo na hununuliwa kwa kutumia
utaratibu wa ununuzi wa pamoja n akusambazwa kwa wakulima kwa kutumia
wakala walioteuliwa na kudhibitishwa na Halmashauri husika”,Alisisitiza
Mhe.Ole Nasha.
EmoticonEmoticon