Dar es Salaam, Tuesday, Aprili 11, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imeingia ubia na Kampuni ya Jackson Group kuzindua App mpya ya mtandao inayofahamika kama Kitabu App ambayo iliyoundwa kwa ajili ya kutoa aina mbalimbali za vitabu (kwa sauti au kuona) kwa wasomaji mbalimbali nchini Tanzania.
App hiyo inaingia sokoni kama suluhisho sio tu kwa wasomaji bali pia kwa waandishi wa vitabu ambao sasa wanaweza kuuza na kufuatilia na mauzo ya vitabu vyao kupitia simu zao za mkononi, kwa kutumia mtandao wa Tigo 4G LTE ambao ni mkubwa, wa kasi na mpana nchini.
Kujumuisha vitabu kwa njia ya sauti katika jukwaa moja inatarajiwa kuwa App hiyo itabadilisha jinsi ambavyo Watanzania watakavyojijengea mazoea kujisomea, hali ambayo itakuwa ni kinyume na kupungua kwa mazoea hayo ambapo kwa kiwango kikubwa kumekuwa kunahusishwa na kuwepo kwa utamaduni mbovu wa kujisomea miongoni mwa wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa App hiyo Meneja Mawasiliano ya Umma wa Tigo Woinde Shisael alisema, “Kampuni yetu inaendelea kuthibitisha kuji kita kwake katika kuwekeza n katika kuboresha utamaduni wa kujisomea nchini Tanzania. Tuna imani kwamba App hii itahamasisha mvuto wa kujisomea miongoni mwa jamii na hivyo kufufua kudorora kwa utamaduni hapa nchini.”
Shisael alisema, “Tayari wateja wetu wengi wanapenda kutumia simu kuchati na marafiki pamoja na wanafamilia,” na kuongeza, “Kupitia Kitabu App tunatoa jukwaa muhimu kwa waandishi, wachoraji na wasomaji kwa ujumla kufikia sehemu rahisi ya kusoma mada mbalimbali kupitia simu ya mkononi.
Akizungumzia kufurahia kwake kushirikiana App hiyo na wateja wa Tigo Shisael alibainisha kwamba hivi sasa wanaweza kuvipata vitabu wavipendavyo wakati wakifanya mambo mengine kwenye simu zao
Akitoa maoni yake kuhusu App hiyo Mkurugenzi wa The Jackson Group, Kelvin Twissa alisema, “ App yetu ya Kitabu App ni ubunifu ulioendeshwa kimkakati ukiwa unahamasishwa na kukua katika kujumuishwa kiteknolojia. Kupitia App hii tunawaruhusu waandishi wa vitabu kufikia kiwango cha hali ya juu cha usoamaji kupitia simu zao za kisasa. Wakati tuna waandeishi wengi wenye vipaji katika aina mbalimbali za vitabu, hali kadhalika kuna uhitaji mkubwa wa uelewa ndani yake.”
Alisema, “Tunaamini kwa kuangalia zaidi katika kukua kwa orodha yetu tunaweza kuleta mabadiliko ndani ya usambazaji kote nchini na kuirudisha tena furaha ya kujisomea kwa Watanznania.”
Twissa aliongeza, “ Kitabu ni App ya kuelimisha, kuburudisha na kuunganisha na mada za kidini. Elimu ni moja ya mitazamo yetu ya msingi, hivyo tunajenga ushirikiano na tunatoa wito kwa taasisi za kielimu kupakua mada zao, kuhifadhi kwa ajili ya kuchapisha na kusambaza vitabu.”
App ya Kitabu App inaweza kupakuliwa bure na kwa hivi sasa inapatikana katika simu za Android ambapo mtumiaji anatakiwa tu kutoa malipo kupitia TigoPesa kwa mada zinazohitajijka na mtu binafsi.
EmoticonEmoticon