WASANII WAAHIDI BURUDANI KALI TAMASHA LA BURUDANI "NYANZA FESTIVAL 2017" JIJINI MWANZA

April 11, 2017
#BMGHabari
Wanatasnia wa burudani hususani wanamuziki mastaa na chipukizi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameahidi kudondosha burudani kali kwenye tamasha la kwanza na la aina yake la Nyanza Festival litakalofanyika April 15 na 16, 2017 Uwanja wa CCM Kirumba.

"Zaidi ya wasanii 30 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa tayari wamethibitisha kupanda jukwaa la Nyanza Festival hivyo niwasihi wapenzi wa burudani wakae tayari kwa burudani hiyo ambapo kiingilio itakuwa elfu tano tu". Amesema Afisa Habari wa tamasha hilo, George Binagi.

Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo nikiwa ni kuukuza na kuuendeleza muziki wa Kanda ya Ziwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »