Aliyevaa Shirt jeupe, Mwenyekiti wa kamati ya kudumu
ya Katiba na Sheria ya Bunge, Mhe. Joseph Mhagama, akimsikiliza
Mhe. Ally Seif Ungano (Mb.) wa Kibiti Mkoani Pwani, anayezungumza kushoto
kwake, wakati wa ziara ya kamati hiyo kisiwani Pemba, wengine katika
Picha ni wabunge ambao ni wajumbe wa kamati hiyo na maofisa wa serikali
zote mbili waliokuwepo katika ziara hiyo.
Pichani kulia ni Mhe.
Saum Sakala, Mbunge viti Maalum (CUF) kutoka katika mkoa wa Tanga, akimuonyesha
Mhe. Twahir Awesu Mbunge wa Mkoani Pemba (CUF) sehemu ya kipande cha
barabara ya Chanjamjawiri, kaskazini Pemba, kilichojengwa chini ya Mradi
wa MIVARF, ambacho kamati ya Bunge ya Katiba na sheria Imependekeza
mradi kuongeza muda ili kukifanyia maboresho ikiwa ni pamoja na kujenga
daraja ili kuhepuka kujaa maji hadsa katika kipindi cha Mvua.
Picha inaonyesha karavati
lililowekwa katika moja ya Barabara ya Chanjamjawiri katika Mkoa wa
Kaskazini Pemba, lililojengwa na mradi wa MIVARF, moja wa mradi wa muungano
wenye lengo la kuboresha miundombinu na kuinua maisha ya wakazi wa Unguja
na Pemba.
Picha ya pamoja imepigwa
katika uwanja wa ndege kisiwani Pemba, ikionyesha wabunge wa Kamati
ya Bunge ya kudumu ya Katiba na Sheria na Baadhi ya watendaji na watumishi
wa Serikali ya SMT na SMZ. (Habari na Picha Zote na Evelyn Mkokoi wa
OMR)
Evelyn Mkokoi-Pemba
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeona
kuna kila sababu ya kumshauri Waziri mwenye dhamana ya katiba na sheria
Mhe.Harrison Mwakyembe kutatua changamoto zinazoikabili tume ya haki
za binadamu kwa kuboresha Ofisi zote za tume hiyo nchini
hususan Ofisi za Pemba na Lindi ili ziweze kutekeleza majukumu yake
ipasavyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe.Joseph Mhagama
(Mb.) Mabada Songea, alisema hayo wakati akifanya majumuisho ya Ziara
ya kamati hiyo kisiwani Pemba.
Baada ya Kupokea taarifa ya Mtendaji Mkuu wa tume
hiyo Nchini Bi. Mary Massey, Mhe. Mhagama alisema Ofisi hizo zinakabiliwa
na changamoto ya rasilimali watu, fedha, vitendea kazi pamoja
samani hivyo kufanya utendaji wa Tume hiyo kisiwani humo kuwa
mgumu.
Pia à lishauri tume hiyo kujengewa uwezo katika eneo
LA utawala bora kama serikali ya awamu ya tano inavyosisitiza.
Awali mbunge wa Bukene Tabora, Mhe. Suleiman Zedi
alisema ufinyu wa bajeti katika tume hiyo unazuia utekelezaji wa mambo
mazuri yaliyokusudiwana serikali, ikiwemo elimu kwa umma kuhusu ukiukwaji
wa misingi ya haki za Binadamu na utawala bora.
Pamoja na hayo imeelezwa kuwa, ufinyu wa bajeti
iliyotengwa Pemba kwa mwaka huu wa fedha unaenda kuisha, umepekelekea
Ofisi Hizo kwa upande wa Pemba kupata kiasi cha sh. 100,000 kwa mwezi
, na wakati mwingine kutopatikana kabisa unasababisha tume kutotekeleza
majukumu yake kwa ukamilifu na pia kushindwa kusogeza huduma zake karibu
zaidi kwa wananchi.
Aidha, ufinyu huo wa Budget umesababisha upungufu
mkubwa wa watumishi kwani tume hiyo imeshindwa kuwalipa watumishi kutoka
Dar es Salaam na kuwahamisha kwenda kwenye matawi ikiwemo tawi LA Pemba
ambalo Lina mfanyakazi mmoja.
Kamati ya kudumu ya katiba na Sheria ya Bunge la
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, imetembelea maeneo ya Mashirikiano
ya Muungano ya Tume ya Haki za Binadanu na Mradi wa MIVARF kisiwani
Pemba, ikiwa na lengo la kuona namna maeneo hayo yanavyofanya kazi kisiwani
humo katika kuimarisha Muungano.
EmoticonEmoticon