Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (kushoto) akiwa
katika kikao cha majumuisho na Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Maggid Mwanga
mara baada ya kukamilisha ziara katika Wilaya hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) akiongea na
Bi. Tatu Rajab mmoja wa wafanyakazi katika Kiwanda cha kutengeneza
chumvi cha Sea Salt. Waziri Makamba alifanya ziara kiwandani hapo
kuangalia changamoto za mazingira.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah mara baada ya kutembelea kijiji
cha Buyuni na kuongea na wananchi.
……………..
Na Lulu Mussa
Saadani – Pwani
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema katika
jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na athari zake Ofisi
yake imeandaa mradi utaonufaisha shule za msingi katika Wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Akiwa Wilayani Bagamoyo Waziri
Makamba amesema kuwa, moja ya changamoto kubwa ya Wilaya ya Bagamoyo ni
ukame unaotokana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, uliopelekea
kupanda kwa kina cha bahari na kusababisha visima vilivyochimbwa pembeni
mwa miji na fukwe za bahari kufukiwa na maji na chumvi.
“Ofisi ya Makamu ya Rais imeamua
kuisadia Wilaya ya Bagamoyo kuchimba visima kumi na saba (17) virefu
kwenye maeneo ambayo yameathirika na kupanda kwa kina cha maji na maeneo
yenye ukame mkubwa” Makamba alisisitiza.
Takribani kila kisima kitagharimu
kiasi cha Shilingi Milioni Hamsini na Ofisi ya Makamu wa Rais pia
itaandaa mfumo wa kuvuna maji katika shule tano mradi utakao gharimu
takribani Milioni mia moja sabini.
Katika hatua nyingine Waziri
Makamba alitembelea Kiwanda cha Sea Salt kilichopo Saadani, Wilaya ya
Bagamoyo kuona namna kiwanda kinavyofanya kazi kwa kuzingatia Sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004.
Waziri Makamba ambaye amewasili
Mkoani Tanga kujionea hali ya mazingira na changamoto za uhifadhi pia
ametembelea Wilaya ya Pangani na kukagua mradi wa ujenzi wa Ukuta wa
Pangani.
Waziri Makamba, amemtaka
mkandarasi anayejenga ukuta wa mto Pangani kampuni ya ( DEZO CIVIL
CONSTRUCTION L.TD ) kukamilisha ujenzi wa ukuta kwa kipindi cha muda wa
miezi kumi, kama mkataba unavyoonyesha na kuzingatia ubora. Ujenzi huo
wa sehemu ya ufukwe wa kaskazini ambao una urefu wa mita 950 ambazo
kati yake mita 550 zipo katika ujenzi wa awali utagharimu kiasi cha
shilingi za kitanzania Bilioni 2.4
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Pangani Bi Zainab Abdalah amemuomba Waziri Makamba kutuma timu ya
wataalamu kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu kwa fukwe pekee iliyoko
katika maeneo ya Tanga DECO ambayo imeathirika kwa kiasi kikubwa na
athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia nchi na haipo katika bajeti kwa
mwaka huu wa fedha.
Ziara ya kikazi wa Waziri Makamba
leo imeingia siku ya pili na ametembelea Kijiji cha Buyuni ambapo pia
alifanya mazungumzo na wakazi wa eneo hilo.
EmoticonEmoticon