Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi,
Abdulrahmani Kaniki akisaluti kwa wimbo wa taifa kabla ya kutoa hotuba
ya ufunguzi wa mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la
wakuu wa Polisi wan chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa
siku mbili unafanyika Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya
kukabili uhalifu unaovuka mipaka. Kushoto ni Mkurugenzi wa upelelezi wa
makosa ya Jinai DCI, Robert Boaz. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la
Polisi.
Naibu Inspekta Jenerali wa
Jeshi la Polisi, Abdulrahmani Kaniki akitoa hotuba ya ufunguzi wa
mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la wakuu wa Polisi wan
chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika
Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya kukabiliana uhalifu unaovuka
mipaka. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi
la Polisi, Abdulrahmani Kaniki akionyesha zawadi kutoka kwa Mkuu wa
Interpol kanda ya kusini (kulia) baada ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa
mkutano wa kamati ndogo za kiufundi za shirikisho la wakuu wa Polisi wan
chi za kusini mwa afrika SAPRCCO. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika
Bagamoyo mkoani Pwani kujadili mikakati ya kukabiliana uhalifu unaovuka
mipaka. Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
……………
Na. Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Wakuu
wa Upelelezi wa makosa ya jinai kusini mwa Afrika wametakiwa kuongeza
ushirikiano katika kubadilishana taarifa za wahalifu na uhalifu unaovuka
mipaka ili kuufanya ukanda wa kusini mwa Afrika kuwa salama.
Wito
huo umetolewa na Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki
mjini Bagamoyo alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili wa Wakuu wa
Upelelezi wa Polisi kutoka Shirikisho la Wakuu wa Polisi kwa nchi za
kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika sambamba na kamati za ufundi za
SARPCCO kwa lengo la kupanga mikakati ya kupambana na uhalifu na
wahalifu.
Kaniki
alisema ili kuwabaini wahalifu kwa urahisi ni vyema ushirikiano wa
kubadilishana taarifa ukafanyika kwa haraka hasa kwa kuimarisha
teknolojia ya habari na mawasiliano na mafunzo kwa maafisa wa Polisi ili
kuwajengea uwezo wa kubaini mapema viashiria vya uhalifu katika maeneo
yao.
Aidha
aliziomba Serikali za nchi wanachama kuendelea kutenga bajeti
zinazokidhi mahitaji ya majeshi ya Polisi ili kuyawezesha kufanya kazi
kwa ufanisi ambapo pia aliyataka majeshi hayo kuzingatia nidhamu ya
matumizi ya fedha zinazotengwa kwa lengo la kuimarisha mifumo ya kuzuia
na kupambana na uhalifu.
Kwa
upande wake Mkurungezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI
Robert Boaz alisema umoja huo utaendelea kuandaa oparesheni za pamoja
katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka unaohusisha wizi wa
magari, dawa za kulevya, biashara haramu ya usafirsishaji wa binadamu,
uharamia, pamoja na ujangili.
Boaz
alibainisha kuwa mkutano huo utajadili kwa kina utekelezaji wa maazimio
yaliyofikiwa katika mkutano wa Wakuu wa Polisi uliofanyika mwezi
Septemba mkoani Arusha pamoja na kuweka mikakati endelevu ya kukabiliana
na uhalifu.
Naye
Mkuu wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (INTERPOL) Kanda ya Kusini
Bw. Mubita Nawa alisema umoja huo umepata mafanikio makubwa kutokana na
oparesheni mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mara kwa mara katika
kukabiliana na uhalifu ambapo amesema biashara haramu ya usafirishaji wa
binadamu bado ni changamoto kwa nchi wanachama.
Shirikisho
la Wakuu wa Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) lipo chini ya Uenyekiti
wa Inspekta Jenerali wa Polisi Tanzania ambapo hivi sasa umoja huo
unaundwa na nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana,
Malawi, Lesotho, Mauritius, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC),
Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland,
Madagascar na Shelisheli.
EmoticonEmoticon