Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds
Media leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo
Dkt. Hassan Abbass.
Katibu wa Kamati ya Kuchunguza
Sakata la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia ofisi za Kituo cha
Televisheni cha Clouds Media, Deodatus Balile akielezea yaliyomo katika
ripoti yao kabla ya kumkabidhi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Nape Moses Nauye (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Nape Moses Nnauye (katikati) akifafanua jambo mbele ya
waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu
tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha
Televisheni cha Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari –
MAELEZO Dkt. Hassan Abbass na Katibu wa Kamati hiyo Deodatus Balile.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Nape Moses Nnauye akikabidhiwa ripoti ya uchunguzi kuhusu
tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha
Televisheni cha Clouds Media na Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi wa
sakata hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Dkt.
Hassan Abbass leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya uchunguzi
wa tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia kituo
cha Televisheni cha Clouds Media ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya
Habari – MAELEZO, Dkt. Hassan Abbass (kushoto) akimwelezea Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye ushahidi wa CCTV
uliombatanishwa katika CD aliyomkabidhi leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari
wakifuatilia makabidhiano ya ripoti ya uchunguzi kuhusu tuhuma za Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuvamia Kituo cha Televisheni cha
Clouds Media leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea taarifa ya kina kuhusu
chanzo, sababu na namna tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul
Makonda alivovamia kituo cha Utangazaji cha Clouds Media akiwa na
walinzi wenye silaha Machi 17, 2017.
Akipokea taarifa hiyo leo Jijini
Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO Dkt.Hassan Abbas ameishukuru
Kamati kwa utulivu wao na kuifanya kazi hiyo kwa utaalamu na umakini
mkubwa huku jamii ikitaka matokeo kwa haraka.
Aidha Mhe. Waziri amesema kuwa ripoti hiyo ataiwasilisha kwa mamlaka husika kwa ajili ya uamuzi na maelekezo.
“Nimeipokea ripoti na
ninawahakikishia kuwa nitaikabidhi ripoti hii kwa wakubwa zangu wao ndo
wenye mamalaka ya kufanya chochote”,Alisema Mhe. Nape.
Kamati aliyoiunda Mhe Waziri
ilikuwa na wajumbe wanne ambao ni Bw.Deodatus Balile kutoka
Jamhuri,Bw.Jesse Kwayu wa Gazeti la The Guardian,Bibi Nengida Johanes wa
Upendo Media na Bibi Mabel Masasi kutoka Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA) walioongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt.Hassan
Abbas .
EmoticonEmoticon