Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu
Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. Waziri
Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea
nyumbani kwake mara baada ya kupata nafuu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa
Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwake Upanga jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa
Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es
Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya
akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ambaye alifika nyumbani kwake Upanga kwa ajili ya kumjulia
hali.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa
Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es
Salaam. PICHA NA IKULU
EmoticonEmoticon