Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akihutubia katika Mkutano wa wadau wa Mfuko
wa Bima ya afya NHIF/CHF
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya
afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda akizungumza katika Mkutano wa wadau wa Mfuko
wa Bima ya afya NHIF/CHF Mkoani Simiyu
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya
afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (kulia) katika Mkutano wa wadau wa Mfuko
wa Bima ya afya NHIF/CHF
Kaimu Mkurugenzi
wa Mfuko wa Bima ya afya Taifa Ndg Leonard Konga akitoa taarifa ya Maboresho ya
huduma kwa wanachama na wadau wa mfuko wa Bima ya afya
Rc Mtaka akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya
afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda akisisitiza jambo katika Mkutano wa wadau wa Mfuko
wa Bima ya afya NHIF/CHF Mkoani Simiyu
Kaimu Meneja wa Bima ya afya Mkoa wa Simiyu ambaye
pia ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Shinyanga Ndg Immanuely
Imani akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF Mkoa wa Simiyu
Rc Mtaka akielezea ruksa ya uwekezaji katika mkoa wa Simiyu ikiwa ni pamoja na ruhusa ya kutoa eneo la ardhi bure kwa yeyeote anayetaka kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu
Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe Tano Mwera akishauri uongozi wa Bima ya afya Taifa kuweka wazi magonjwa yasiyotibiwa kwa kutumia Bima ya afya huku akitilia mkazo kadhia ya unyanyapaa wanayokumbana nayo watumiaji wa Bima ya afya
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya
afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda (kushoto) akizungumza jambo na
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka katika Mkutano wa wadau wa
Mfuko
wa Bima ya afya NHIF/CHF alipozuru katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Wadau wa
Mfuko
wa Bima ya afya NHIF/CHF wakisikiliza kwa makini huku wengine wakipata nafasi ya kuuliza maswali kwenye mjadala katika Mkutano huo
Na Mathias Canal, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amesema kuwa ushirikiano baina
ya Ofisi yake,Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na wananchi
kwa ujumla utaufanya mkoa huo kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi kujiunga
kwenye mfuko wa Bima ya Afya kama ambavyo lengo la Bodi na wizara ya
afya limekusudiwa Kwani wananchi kujiunga na Mfuko wa Bima ya afya ndio
mbinu pekee rahisi na kisasa katika matibabu duniani kote.
RC
Mtaka ameyasema hayo wakati akihutubia katika Mkutano wa wadau wa Mfuko
wa Bima ya afya NHIF/CHF, Mkutano uliokuwa na madhumuni ya kubaini
changamoto zinazowakabili wananchi wanaotumia Mfuko wa Bima ya afya
sawia na kutoa elimu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Bima ya afya.
Ameeleza kuwa kujiunga na mfuko huo ni muhimu kwa wananchi kwani
watapunguza gharama kubwa wakati wa matibabu kwa wale ambao hawajajiunga
kwani wanapaswa kutambua kuwa ugonjwa hauna Siku rasmi ya kuingia
mwilini unawakumba watu wakati wowote pasina kubisha hodi.
Katika
kufikia dhamira ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John
Pombe Magufuli ili kuwa na Tanzania ya viwanda Mkuu Huyo wa Mkoa wa
Simiyu ameiomba Bodi ya Mfuko huo wa Bima ya afya kuanzisha ofisi za
Mkoa kwani watapatiwa eneo la ujenzi pasina kulipia.
Hata hivyo
amesema kuwa kwa yeyote anayetaka kuwekeza kwa kujenga kiwanda cha
kutengeneza Dawa na vifaa tiba atapatiwa eneo Bure kwa ajili ya
kuanzisha kiwanda hicho.
Awali akitoa taarifa ya Maboresho ya
huduma kwa wanachama na wadau wa mfuko wa Bima ya afya Kaimu Mkurugenzi
wa Mfuko wa Bima ya afya Taifa Ndg Leonard Konga amesema kuwa Mfuko wa
Bima ya Afya ni Taaisi ya umma iliyoundwa kwa mujibu wa sheria sura Na
395 TL 2002 ambapo ni matokeo ya utekelezaji wa Sera ya mabadiliko
katika sekta ya afya iliyoanza kutekelezwa kuanzia miaka ya 1990.
Mfuko huo umeanzishwa kwa dhamira ya kutoa Bima ya afya kwa makundi
mbalimbali ya wananchi, Kujenga uwezo wa kifedha kwa vituo, Kushirikisha
sekta binafsi katika kuharakisha maendeleo ya sekta ya afya.
Konga amesema kuwa mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Bima ya afya
yanategemea kila mdau kutimiza wajibu wake kwani mazingira ya kiutendaji
ni kusimamia na kutekeleza miongozo na maagizo ya serikali kupitia
wizara yenye dhamana ya kusimamia upatikanaji wa huduma za afya.
Amebainisha kuwa lengo mahususi katika utekelezaji wa mpango wa Mfuko wa
Bima ya afya ni kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata huduma za afya
kuanzia ngazi ya Zahanati hadi ngazi ya hospitali ya Mkoa, Kuongeza wigo
mpana zaidi kwa watanzania wanaopata huduma za matibabu kupitia Bima ya
Afya.
Naye Kaimu Meneja wa wa Bima ya afya Mkoa wa Simiyu ambaye
pia ni Meneja wa Mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Shinyanga Ndg Immanuely
Imani akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za NHIF Mkoa wa Simiyu
amezitaja changamoto zinazowakabili ikiwa ni pamoja na Upungufu wa dawa
katika baadhi ya vituo, Ukosefu wa vifaa tiba na ubovu wa majengo,
Baadhi ya waajiri kuchelewesha madai, Watoa huduma wachache kuwasilisha
madai yenye kutiliwa shaka na mwitikio mdogo wa wananchi kujiunga na
NHIF/CHF.
Sambamba na hayo pia ameelezea matarajio ya Mfuko wa
Bima ya afya katika Mkoa wa Simiyu kuwa ni pamoja na kuelimisha watoa
huduma kutumia fedha za uchangiaji kwa ajili ya kununulia dawa, kuhimiza
watoa huduma kuomba mikopo ya vifaa tiba, ukarabati, dawa na
vitendanishi.
Matarajio mengine ni pamoja na kuendelea kuimarisha
ukaguzi wa waajiri ili kutoa michango sahihi kwa wakati, Kuimarisha
mifumo ya ulipaji madai ili kuzuia malipo ya madai yasiyo halali na
kuendelea kushirikiana na Halmashauri katika kuhamasisha jamii kujiunga
na Mfuko wa Bima ya afya.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya
afya Taifa (NHIF) Bi Anne Semamba Makinda Amesema kuwa Bodi yake
imekusudia kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi sawia na kupinga
vikali lugha mbovu zitolewazo na baadhi ya watoa huduma katika sekta ya
afya dhidi ya wananchi wanaoenda kupata matibabu katika Zahanati, Vituo
vya afya, Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa.
Amesema katika
maeneo mengi waliyopita wamebaini kuwa wananchi wengi wametumia fedha
zao kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya lakini wanapoenda kuhudumiwa
wanakumbana na matusi pasina huduma bora.
Bi Makinda amesema kuwa
wanaendelea na utaratibu wa kubaini zahabati, kituo cha afya ama
Hospitali zinazokiuka utaratibu Na baada ya kubainika tu watachukuliwa
hatua Kali za kisheria.
Hata hivyo ameeleza jinsi ambavyo mtandao
wa matibabu wa serikali ulivyo mzuri kwani unaanzia ngazi ya Kijiji,
Kata, Wilaya, Mkoa hadi Taifa.
Bodi hiyo imeahidi kufungua Ofisi
za mikoa mipya ya Njombe, Katavi, Geita huku wakiahidi pia kuanza ujenzi
na kufungua ofiai katika Mkoa wa Simiyu baada ya kupewa eneo la ujenzi
Bure na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Antony Mtaka.
EmoticonEmoticon